BAGHDAD: 80 walipuliwa nchini Irak
20 Juni 2007Matangazo
Polisi nchini Irak imethibitisha kuwa watu wapatao 80 wameuawa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya lori karibu na msikiti wa washia mjini Baghdad.
Shambulio hilo limefanyika siku mbili tu baada ya amri ya kudhibiti usalama kuondolewa.katika mji huo.Mamia ya watu wengine walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Katika tukio jingine majeshi ya Marekani yaliwaua watu 23 waliotuhumiwa kuwa wapinzani. Maalfu ya majeshi hayo yameanzisha kampeni kubwa inayoelekezwa dhidi ya wapinzani wa kisuni na wapiganaji wa al-Kaida kaskazini na kusini ya Baghdad ambako wapiganaji hao wamekimbilia.