BAGHDAD : 25 wauwawa wakiwemo wanajeshi 10 wa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : 25 wauwawa wakiwemo wanajeshi 10 wa Marekani

Takriban watu 25 wameuwawa nchini kote Iraq katika mashambulizi kadhaa.

Watu wanane waliuwawa na wengine 40 kujeruhiwa wakati mabomu yaliovurumishwa na mizinga kupiga soko katikati ya Baghdad. Maduka na magari kadhaa yameharibiwa kwenye soko hilo la Harag lilioko karibu na majengo kadhaa ya seraikali na ambalo huko nyuma lilikuwa limelengwa kwa miripuko kadhaa ya mabomu.

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wake 10 wameuwawa katika matukio manne tafauti bila ya kutowa ufafanuzi zaidi.Maafa hayo yanaifanya idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa tokea uvamizi ulioongozwa na Marekani nchini humo hapo mwaka 2003 kufikia 2,899.

Polisi ya Iraq pia iligunduwa maiti 45 za wanaume waliouwawa kwa kupigwa risasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com