BAGHDAD : 18 wamefariki baada ya kupondwa na gari | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : 18 wamefariki baada ya kupondwa na gari

Dereva wa gari kubwa la mizigo akiwa katika mwendo wa kasi amewaponda umma wa watu waliokuwa wakisubiri kwenye kituo cha basi katika mji wa kusini wa Baghdad na kuuwa watu 18 na kujeruhiwa wengine wanane.

Gari hilo liliwaponda watu hao huko Al-Wahda kilomita 35 kusini mwa mji mkuu wa Baghdad wakati wakisubiri basi kuelekea mji mkuu.Inafikiriwa kwamba hiyo ilikuwa ni ajali.

Katika soko la Baghdad kumetokea mripuko leo hii na kuuwa watu 38 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com