1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock: Sina nia ya kugombea ukansela

11 Julai 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock amesema hana mpango wa kugombea tena nafasi ya ukansela katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

https://p.dw.com/p/4i9dN
Berlin, Ujerumani | Siasa | Annalena Baerbock Waziri wa Mambo ya Nje
Annalena Baerbock Waziri wa Mambo ya Nje Ujerumani akizungumza na waandishi wa habari.Picha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Katika matamshi yake yaliyorushwa jana Jumatano kwenye televisheni, Baerbock amesema wajibu wake wa kisiasa kwa sasa ni kuzingatia zaidi masuala ya kidiplomasia wakati huu ambapo kuna migogoro mingi, na sio kampeni za uchaguzi.

Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani, CNN kwamba ataendelea kutumia nguvu zake zote kama waziri wa mambo ya nje kujenga uaminifu na ushirikiano kwa sababu washirika wengi duniani kote na Ulaya wanategemea hilo.

Soma pia:Baerbock: weka himizo kwa Israel kujizuia dhidi ya Hezbollah

Baerbock alikuwa mgombea wa kwanza wa ukansela wa chama cha Kijani kinachotetea mazingira, katika uchaguzi wa mwaka 2021, ambapo kilipata matokeo ya kihistoria ya asilimia 14.7 ya kura.