1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba wa muziki wa Jazz, Hugh Masekela afariki dunia

Isaac Gamba
23 Januari 2018

Mpiga Tarumbeta maarufu nchini Afrika Kusini Hugh Masekela anayefahamika kama baba wa muziki wa Jazz amefariki dunia baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya tezi dume

https://p.dw.com/p/2rLuH
Hugh Masekela
Picha: Imago/Future Image

Mpiga Tarumbeta maarufu nchini Afrika Kusini Hugh Masekela anayefahamika kama baba wa muziki wa Jazz amefariki dunia baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani ya tezi dume. 

Hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.  Masekela amabaye hadi kifo chake alikuwa na umri wa miaka 78 katika kipindi chake cha zaidi ya miongo mitano kwenye fani hiyo ya muziki alijijengea umaarufu kimataifa kutokana na utunzi wa nyimbo zake za muziki  wa Jazz ukiwemo wimbo  uliotumika katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.

Hugh Masekela alitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwanza fainali hizo kufanyika barani Afrika.