1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu Benedicti wa 16 azidi kukosolewa

Saumu Mwasimba4 Februari 2009

-

https://p.dw.com/p/GmuM
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Benedict 16Picha: picture-alliance/ dpa

Hatua ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikti wa 16 ya kumrudisha kundini askofu Richard Williamson aliyekuwa ametengwa baada ya kukanusha kutokea kwa mauaji makubwa ya wayahudi ya Holocoust imezusha hasira miongoni mwa viongozi mbali mbali nchini Ujerumani.

Viongozi maarufu wa kinisa hilo wanasiasa na hata wahariri wa magazeti ya humu nchini wameikosoa vikali.Kansela Angela Merkel ni miongoni mwa wanasiasa waliokosa hatua hiyo.

Kiasi cha miaka minne iliyopita baada ya wajerumani kujivunia kuchaguliwa kwa kiongozi wa kanisa katoliki mzaliwa wa nchi hiyo Kardinali Ratzinger,baba mtakatifu Benedickti wa 16 sasa kiongozi huyo wa kidini amewatumbukia nyongo kutokana na hatua yake ya hivi karibuni ya kumrudisha tena kundini askofu Richard Williamson aliyekana kwamba mauaji ya wayahudi ya Holocoust yalitokea. Viongozi mbali mbali na wajerumani kwa jumla wameikosoa hatua ya Papa wakisema haistahili kabisa.Askofu huyo alirudishwa kundi pamoja na wenzake watatu waliokuwa wametengwa na kanisa hilo.

Msemaji wa kanisa hilo Farther Federico Lombardi akizungumza na kituo cha radio cha humu nchini cha ARD amemtetea baba mtakatifu akisema maoni na mwelekeo wa baba mtakatifu Benedikti wa 16 yamefika mwisho akaongeza kusema.

''Anachofikiri baba mtakatifu juu ya mauaji ya Holocoust ni wazi kimezusha matatizo makubwa katika sinagogi mjini Koln hapo tarehe 19 Agosti mwaka 2005 na tena katika kambi ya mateso ya Auswitz hapo tarehe 18 mai mwaka 2006 na vile vile katika hotuba yake siku tatu baadae na mwishowe mapema mwishoni mwa hotuba yake ya tarehe28 Januari amekuwa akitoa matamshi yanayoeleweka vibaya.''

Gazeti maarufu la humu nchini la Bild ambalo lilimsifu sana kardinali Ratzinger baada ya kuchaguliwa kuwa baba mtakatifu limemkosoa sana katika uhariri wake na kuandika kwamba papa amefanya makosa makubwa na hasa ikizingatiwa yeye ni mjerumani anazidi kuyaharibu mambo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia amezungumzia msimamo wake kuhusiana na hatua hiyo ya baba mtakatifu akisema ni suala la msingi kuwa uamuzi kama huo unapotolewa na Vatican basi ni wazi kwamba hisia za wanaokanusha mauaji hayo ya Holocoust zinaongezeka na kuonekana kama ni jambo linalowezekana.Kadhalika kansela Merkel amesema anahitaji kupewa ufafanuzi zaidi na makao makuu ya Vatican juu ya suala hili. Hata hivyo Vatican haikuchelea kumjibu Kansela Merkel,imesema msimamo wa Baba mtakatifu juu ya mauaji ya wayahudi ya Holocoust hauna utata.Na kuwa hakuna walakini kwamba papa anamlaani yoyote anayekanusha juu ya kutokea kwa mauaji hayo.

Msemaji wake Father Federico ameongeza kusema kwamba,

''Inaniwia vigumu sana hivi sasa kusema juu ya suala hili bila kuzusha mvutano wowote pia hakuna uwazi wa kuzungumziwa juu ya mauaji hayo kuliko inavyozungumziwa hivi sasa.''

Papa pia amekosolewa sana na viongozi wa kikatoliki nchini Ujerumani Cardinarli Karl Lehman ameelezea kitendo cha papa kuwa ni janga kubwa.Kwa upande mwingine waziri wa zamani wa mambo ya nje Hans Dietrich Genscher ameandika katika gazeti moja la humu nchi kwamba watu wanaweza kujivunia Marehemu baba mtakatifu John Paul wa Pili,Katika shughuli ya kuchaguliwa papa mpya tulisema kwamba sisi ni papa, lakini kwa hivi sasa anasema ni kinyume chake.''