AWJA: Maelfu ya wairaki wamiminika kaburini kwa Saddam | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AWJA: Maelfu ya wairaki wamiminika kaburini kwa Saddam

Maelfu ya wairaki leo wamemiminika mjini Awja ambako rais wa zamani wa Irak Saddam Hussein amezikwa. Jamaa zake na waombolezaji walihudhuria mazishi ya kiongozi huyo mda mfupi kabla alfajiri, karibu na mjini Tikrit, yapata kilomita 130 kaskazini mwa Baghdad.

Sheik al Nidaa, kiongozi wa mbari ya Albu-Nassir ya Saddam Hussein, amelaani jinsi Saddam alivyonyongwa na akasema anakichukulia kitendo hicho kama uhalifu. Aidha kiongozi huyo amesema waliupokea mwili wa Saddam bila matatizo yoyote akisema kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa waziri mkuu wa Irak na mkurugenzi wa ofisi yake.

Amethibitisha kuwa mwili wa Saddam ulikuwa umeoshwa na kufungwa nguo kwa mujibu wa mafunzo ya dini ya kiislamu na wala haukuwa na alama zozote za mateso. Kwa mujibu wa ukanda mpya wa video Saddam Hussein alijibizana na watu waliokuwa wamekusanyika kushuhudia akinyongwa. Baadaye Saddam alisema ombi la kiislamu kabla kufa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com