AU yasaka suluhu ya mgogoro wa wakimbizi Afrika | Matukio ya Afrika | DW | 09.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

AU yasaka suluhu ya mgogoro wa wakimbizi Afrika

Watu wengi wanaokimbia hali za migogoro hawawezi kuondoka nchini mwao. Waandishi wa DW wamechambua migogoro ya wakimbizi Afrika: Wakimbizi wa ndani ndiyo wako hatarini zaidi.

Wakimbizi wa Afrika wanahama. Wanakimbia kwa miguu, magari na hata boti ndani ya mataifa yao na kuvuka mipaka kuokoa maisha yao. Hata mwaka 2018 bara hilo limerikodi idadi kubwa ya wakimbizi, lakini Umoja wa Afrika hauna uwezo wa kudhibiti.

Wiki hii Umoja wa Afrika unajadili suala hili: Wakimbizi, warejeao na wakimbizi wa ndani: Kuelekea suluhisho la kudumu kwa uhamaji wa kulaazimishwa barani Afrika". Ni suala ambalo lilipaswa kuwa kwenye ajenda muda mrefu uliopita, anasema Erol Yayboke, naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kimkakati na kimataifa, CSIS.

"Hatua ya Umoja wa Afrika kuizingatia mada hii ni ya kutia moyo. Sisi Wamarekani wa Waulaya tunaamini kwamba Afrika inatusukumia maboti ya wakimbizi, lakini hilo siyo kweli. Watu wengi zaidi wanabakia barani humo. Na sasa ni juu ya Umoja wa Afrika, kwa sababu matatizo ya Afrika yanapaswa kutatuliwa na viongozi wa Afrika, na hilo lina umihimu wa kipekee."

Mwaka 2018 shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa lilirekodi watu milioni 30 wenye uhitaji barani Afrika. Idadi hiyo inajumlisha karibu wakimbizi milioni 7.5, waomba hifadhi 630,000, watu milioni moja wasio na utaifa na karibu nusu milioni ya wakimbizi wanaorejea. Lakini kundi kubwa limebakia kuwa wakimbizi wa ndani mwaka 2018. Zaidi ya Waafrika milioni 18 wamekosa makaazi ndani ya mataifa yao, wakikosa uwezo au kutokuwa tayari kuondoka kwa sababu mbalimbali.

Infografik Internally displaced people in Afrika SW

"Watu wanapopoteza makaazi yao wana kawaida ya kubakia katika hali hiyo. Hii inafungana na hali ya pili kwamba watu waliogeuka wkaimbizi wa ndani siyo wale tu waiotaka kwenda nyumbani. Ni wale ambao hawakuwa na uwezo wa kuendelea zaidi. Hivyo mara nyingi tuwafikia wakimbizi kama watu walioko katika hatari kubwa zaidi duniani. Lakini ukweli ni kwamba kundi la wakimbizi wa ndani ndiyo liko katika hatari kubwa zaidi duniani," anasema Erol Yayboke.

Matumaini hewa ya kurejea haraka

Hali ni mbaya zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako raia milioni 4.4 waliapa kisogo makaazi yao mwaka 2017, lakini badala ya kuanza maisha mapya nje ya nchi, watu hao walikwenda kwenye maeneo yalio karibu na nyumbani kwao. Wacongo wengine 815,000 waliondoka nchini humo mwaka 2018, ambapo asilimia 30 kati yao walikwenda Uganda, asilimia 10 Rwanda na asilimia 8 walikimbilia Tanzania.

"Hii inatokana kwa sehemu na ukubwa wa nchi unaowafanya wengi kushindwa kusafiri", anaeleza Yayboke na kutolea mifano ya uasi mashariki mwa Congo, machafuko katika maeneo ya kusini na mripuko wa Ebola upande wa kaskazini mashariki. "Hakuna mahala watu hao wanaweza kukimbilia."

Mwenendo huu hauko tu nchini DRC: Nchini Somalia ambako kuna watu milioni 2.7 waliokosa makaazi, na Nigeria yenye waathirika milioni 2, idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi pakubwa idadi ya wakimbizi wa nje. Kuna sababu mbili za hilo: Wengi wao wanatumaini kuweza kurudi nyumbani wakati mmoja, jambo ambalo kwa bahari mbaya halitokei kwa wengi wao.

Na sababu ya pili ni kwamba watu hawa hawana uwezo wa kuondoka nchini mwao. Na hilo ndiyo linawafanya kuwa watu walioko katikahatari kubwa zaidi kwa wanalaazimika kuishi kama wakimbizi wa ndani kwa muda mrefu. Wako katika hatari kubwa, anasema Yayboke.

Afrika Flucht Flüchtlinge aus Niger und Nigeria (Getty Images/AFP/S. Ag Anara)

Kundi la wakimbizi hasa kutoka Niger na Nigeria, wakimpumzika Januari 22, 2019 kabla ya kuendelea na safari kuvuka jangwa la kaskazini mwa Niger kwenda mpaka wa Libya.

Wanaorejea hugeuka wakimbizi wa ndani

Waafrika wengi wanakabiliwa na mustakabali wa mashaka kama wakimbizi. Umoja wa Afrika unataka kuwasaidia, lakini mapaka sasa haujafanikiwa, anasema Kathleen Newland, mwasisi mwenza wa taasisi ya sera ya uhamiaji na mjumbe wa bodi wa Wakurugenzi ya UNHCR. Anasema Umoja wa Afrika unapaswa kuruhusiwa kujaribu lakini anaongeza kuwa hauna uwezo wa kuyaambia mataifa nini cha kufanya ili kuweza kubadili hali.

"Mamlaka yao yana mipaka juu ya nini wanaweza kufanya. Hatuwezi kusema umeshindwa, lakini ni kwamba huna zana na rasilimali na ushawishi kuziambia nchi nini cha kufanya na hauna mamlaka yoyote ya kulaazimisha jambo."


"Umoja wa Afrika ni mdau muhimu ambaye anapaswa kupambana dhidi ya mataifa makubwa na yenye nguvu zaidi", anasema Yakobe. Anasema umoja huo hautatuwi matatizo ya wakati huo kikamilifu na hapohapo yanazuka mengine. "Tatizo kubwa zaidi la wakimbizi wa ndani linabaki kuwa hawalindwi na sheria ya kimataifa. Mkimbizi anaweza kuomba hifadhi, na mtu aliekosa makaazi hawezi." Zaidi ya hayo, "jumuiya ya kimataifa haiwezi kumlinda kwa sababu serikali haiwezi kuruhusiwa na serikali kuingia nchini kuwasaidia watu", anasema Yayboke.

Kwa sasa kuna wakimbizi wengi wa ndani, hasa katika mataifa ya Afrika Mashariki. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tatizo hilo linaonekana kuzidi kuiathiri kanda ya Afrika Magharibi: Wakati mwaka 2017 Mali ilikuwa na idadi ndogo ya wakimbizi 38,000 wa ndani, mwaka mmoja baadae idadi hiyo iliongezeka karibu mara tatu zaidi. Hali kama hiyo inaweza kushuhudiwa pia nchini Burkina Faso. "Hii haishangazi pia", anasema Yayboke. Kwa maoni yake, hii inatokana na ongezeko la makundi ya kigaidi kama vile Al Qaeda katika Magharibi (AQIM).

Newland anasisitiza kwamba wakimbizi wanaorejea mara nyingi hugeuka wakimbizi wa ndani wanapowasili nyumbani. Kwa wengi ni suala lisilo na mjadala kurudi katika mji wao wa nyumbani na watu wanavutiwa na maeneo mengine. Idadi ndogo tu ya watu 400,000 walirejea kwenye mataifa yao mwaka 2018, jambo ambalo Umoja wa Afrika unataka kulifanyia kazi. Idadi halisi yumkini ni ndogo zaidi, anasema Yaykobe. "Watu hawarudi palipo bado na matatizo". Urejeaji wa kulaazimishwa kwa upande mwingine, unakiuka sheria ya kimataifa. "Mtu aliefukuzwa katika ardhi yake hawezi kulaazimishwa tena kurudi kinyume na matakwa yake.

Infografik Number of refugees and asylum seekers living in destination country SW

Uganda yanedelea kuwa ruwaza

Waafrika ambao hukimbilia ng'ambo ndiyo suluhisho, wanakimbilia zaidi katika mataifa jirani. Nchi ambayo watu wengi huondoka ni Sudan Kusini, taifa changa kabisaa linalokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na njaa, ambalo watu milioni 2.3 wamekimbia na kuelekea hasa Uganda, Ethiopia na Sudan. Mataifa haya matatu pia ndiyo kimbilio la juu la wakimbizi wa Kiafrika. Uganda ndiyo iliongoza mwaka 2017 kwa kupokea wakimbizi milioni 1.4. Ikilinganishwa na miaka mitatu ya nyuma, idadi hiyo ilikuwa chini ya milioni moja na nusu.

Newland anafafanua kuwa Uganda inawawia rahisi wakimbizi kuingia, kutokana na ukarimu wake kwao, na sera yake ya kuwapatia ardhi ili kujitegemea. Zaidi ya hapo, baadhi ya wakimbizi wanaishi kwenye kambi kwa miaka mingi. Vizazi vimezaliwa huko, jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi. Lakini Newland anasema inazidi kuwa vigumu kwa Uganda kuendeleza sera hii ya wazi.

Ni safari ndefu kwa Umoja wa Afrika kukabiliana na matatizo haya yote, Newland alisema. "Mfumo wa kisheria unapaswa kuwekwa ili kuwalinda watu walikosa makazi yao Afrika." Nadhani Umoja wa Afrika utajitahisi kupatanisha mataifa kama Ethiopia na Eritrea. Wana nia na mikakati mizuri, lakini hali ya wakimbizi wa Afrika ni changamoto kubwa ambayo jambo moja linahitajika juu ya yote: Muda."

Mwandishi: Silja Katharina Fröhlich'
Tafsiri: Iddi Ssessanga
Mhariri: Mohammed Khelef