Atletico yalipiza kisasi dhidi ya Real Madrid | Michezo | DW | 25.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Atletico yalipiza kisasi dhidi ya Real Madrid

Atletico Madrid ya Uhispania imepata kiasi kunusa ulipizaji kisasi kutokana na kushindwa katika fainali ya Champions League msimu uliopita dhidi ya Real Madrid. Hivyo wajipiga kifua mjini Madrid

Hii ni baada ya vijana hao wa kocha Diego Simeone kupata ushindi mnono wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa hao jana katika uwanja wa Vicente Calderon na kunyakua kombe la "Super Cup" nchini Uhispania.

Alikuwa mchezaji wa zamani wa Bayern Munich Mario Mandzukic aliyepeleka kilio kwa Real Madrid baada ya kupachika bao la ushindi sekunde 90 tu baada ya kuanza kwa pambano hilo la wababe wa mji Madrid.

Kocha wa Real Carlo Anceloti alimuweka Cristiano Ronaldo benchi kutokana na maumivu ya paja yaliyosababisha kutolewa na mapema katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 wiki moja iliyopita.

Hata hivyo , mshambuliaji huyo Mreno hakuweza kuvunja ukuta wa Atletico uliojipanga vyema wakati wakiyaweka matumaini ya Real mbali na kunyakua mataji sita msimu huu.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe /rtre

Mhariri: Yusuf Saumu