1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assad asisitiza hatajiuzulu

19 Mei 2013

Rais wa Syria Bashar al Assad amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya mwisho wa kipindi chake madaraka mwaka 2014, wakati bomu lililotegwa katika gari liua watu watatu katika mji mkuu Damascus.

https://p.dw.com/p/18aYm
ARCHIV - Der syrische Staatspräsident Baschar al-Assad (Archivfoto vom 12.02.2013) befürchtet eine militärische Intervention des Westens in seinem Land. «Die Vorwürfe gegen Syrien bezüglich Chemiewaffen und die Forderungen nach meinem Rücktritt ändern sich jeden Tag», sagte Al-Assad in einem am 18.05.2013 veröffentlichten Interview der staatlichen argentinischen Nachrichtenagentur Télam. EPA/SANA / HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Baschar al-AssadPicha: picture alliance/dpa

"Kujiuzulu ni sawa na kukimbia", Assad amesema katika mahojiano na gazeti moja la Argentina la Clarin wakati alipoulizwa iwapo anaweza kufikiria kujiuzulu kama waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry anavyotaka.

"Sifahamu iwapo Kerry ama yeyote mwingine amepata madaraka ya watu wa Syria kuzungumzia kwa niaba yao juu ya nani anapaswa kuondoka madarakani na nani anapaswa kubaki. Suala hilo litaamuliwa na watu wa Syria katika uchaguzi wa rais mwaka 2014.

Mkutano wa upatanishi

Hata hivyo amesema kuwa anakaribisha juhudi za Marekani na Urusi za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vilivyodumu kwa muda wa miaka miwili sasa.

Family members of Mohammed Aboud, chant slogans against the Sunni-dominated Free Syrian Army rebel group and the al-Qaida-affiliated Jabhat al-Nusra during his funeral in Basra, Iraq's second-largest city, 340 miles (550 kilometers) southeast of Baghdad, Iraq, Friday, May 17, 2013. Hundreds of Iraqis in Basra, have attended the funeral of two Shiite fighters killed in Syria. Relatives of Aboud say he was killed by a sniper fire near the shrine of Sayida Zeinab outside the capital of Damascus five days ago. Arabic writing on coffin reads, “Sigh in grief, Zeinab.” (AP Photo/ Nabil Al-Jurani)
Raia wakishughulika wakati wa shambulio la bomuPicha: picture-alliance/AP

Marekani na Urusi zinajaribu kuitisha mkutano wa kimataifa wa amani mjini Geneva ambao utawaleta pamoja wajumbe wa serikali na waasi wanaopigana kuuondoa utawala wa Assad.

"Tumepokea hatua ya Urusi na Marekani kwa vizuri na tuna matumaini kuwa kutakuwa na mkutano wa kimataifa kuwasaidia Wasyria kumaliza mzozo wao." Gazeti la Clarin limemnukuu Assad akisema.

Ameongeza hata hivyo kuwa, " Hatuamini kuwa mataifa mengi ya magharibi yanataka kweli suluhisho nchini Syria. Na hatufikiri kuwa mataifa yanayowasaidia magaidi yanataka suluhisho katika mzozo huu."

People stand on the site of a car bomb explosion on May 11, 2013 near the town hall of Reyhanli, just a few kilometres from the main border crossing into Syria, killing 18 people in one of the deadliest recent attacks in the volatile area. Two explosive-laden cars blew up in a small Turkish town near the volatile border with Syria on Saturday. The attacks in the town of Reyhanli, just a few kilometres from the main border crossing into Syria, come amid increasingly bellicose criticism by Ankara of the regime in Damascus. AFP PHOTO/ IHLAS NEWS AGENCY ***TURKEY OUT*** (Photo credit should read STR/AFP/Getty Images)
Hali inazidi kuwa mbaya kila siku nchini SyriaPicha: STR/AFP/Getty Images

Magaidi nchini Syria

Syria inawaita waasi ambao wamekuwa wakipigana kuuondoa utawala huo kuwa ni " magaidi".

Jana Jumamosi (18.05.2013) televisheni ya taifa imewashutumu wale iliyowaita magaidi kwa kuripua bomu lililokuwa limetegwa katika gari katika kitongoji cha kaskazini mwa mji mkuu Damascus , ikisema kuwa kiasi watu watatu wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa.

Shirika hilo la televisheni la taifa limesema bomu hilo liliwekwa katika gari katika kitongoji cha Rokn Eddin na kwamba kikosi cha kutegua mabomu kilipelekwa katika eneo hilo kutegua bomu jingine.

Shambulio la bomu

Televisheni ya taifa imesema kuwa shambulio hilo la bomu lilitokea katika sehemu ya kuegesha magari karibu na shule na msikiti.

epa03498499 A handout photo made available by the Syrian Arab News Agency (SANA) shows a damaged car at the site where an explosive device went off in al-Zahera neighborhood in Damascus, Syria, 06 December 2012. A car bomb exploded outside the offices of the Syrian Red Crescent in the capital Damascus, killing at least one person, reported state television. EPA/SANA/HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES
Shambulio la bomu katika eneo la kuegesha magari mjini DamascusPicha: picture-alliance/dpa

Kituo hicho kilirusha picha hewani za waokoaji wakiweka miili ya wahanga iliyoharibika katika mifuko maalum , madimbwi ya damu , mabaki ya magari yaliyoharibiwa na mripuko huo pamoja na basi la abiria lililoharibiwa vibaya, wakati wanajeshi wa serikali wakiwa wanaangalia.

Shirika la kuangalia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake makuu mjini London pia limeripoti kuhusu shambulio hilo la bomu, lakini limetoa idadi ya juu ya watu waliofariki kuwa ni wanane na wengine 10 wamejeruhiwa.

Taarifa imesema kuwa shambulio hilo la bomu lililenga magari ya jeshi la serikali, na kuuwa wanajeshi wanne wa kawaida na raia wanne.

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulio hilo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Sudi Mnette