ARUSHA:Mazungumzo yaendelea kati ya waasi wa darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 03.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ARUSHA:Mazungumzo yaendelea kati ya waasi wa darfur

Makundi ya waasi ya Darfur nchini Sudan wanakutana mjini Arusha nchini Tanzania ili kwa mazungumzo yanayolenga kufikia mwafaka kufuatia hatua ya kuidhinisha azimio la Umoja wa mataifa la kuepeleka kikosi cha kulinda amani kilichoimarishwa kwenye eneo la Darfur.Mkutano huo unafadhiliwa na Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Mataifa na unaazimia kuwashawishi waasi kufanya mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan.Dr Salim Ahmed Salim ni mjumbe wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo hayo

''Makubaliano ya Darfur kati ya serikali na waasi yalifikiwa mwaka jana lakini kuidhinishwa na kundi moja tu kati ya makundi matatu yanayojadiliana na serikali.''

Wakati huohuo ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Sudan AMIS unalaani kitendo cha kutishwa kwa majeshi yao na kundi la waasi waliojihami kwa silaha nzito nzito.Vitisho hivyo vimetokea wiki hii katika eneo la darfur.

Kulingana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur,Jan Eliasson juhudi za kisiasa za kumaliza mgogoro wa Darfur zimefikia hatua muhimu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com