Arusha. Tanzania. Padre ahukumiwa kuhusiana na mauaji nchini Rwanda. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Arusha. Tanzania. Padre ahukumiwa kuhusiana na mauaji nchini Rwanda.

Mahakama ya umoja wa mataifa inayowahukumu wahalifu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda imemhukumu padre wa kanisa Katoliki kwa mauaji kutokana na kuhusika kwake katika mauaji ya mwaka 1994. Padre Athanase Seromba ni mchungaji wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hiyo imemhukumu kwenda jela kwa miaka 15, kutokana na kumpata na hatia kwa mashtaka mawili kati ya manne.

Seromba ambaye ni Mhutu anatuhumiwa kwa kuamuru kanisa lake kuvunjwa na mabuldoza ambapo Watutsi 2,000 waumini walikuwa wamejihifadhi mwezi Aprili 1994, na kuuwa watu wote waliokuwamo. Amedai kuwa alikuwa mchungaji tu na hakuwa na uwezo wa kuzuwia mauaji hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com