1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal kujipima nguvu na Palace

Sekione Kitojo
10 Aprili 2017

Arsenal London ina mtihani mkubwa kujaribu kujiinua kufika katika nafasi ya kucheza katika Champions League msimu ujao

https://p.dw.com/p/2b0Zw
UK | Fußball | Hull City v Arsenal
Mlinzi wa Arsenal Per Mertesacker Picha: picture-alliance/empics/S. Bellis

Ligi  ya  England , Premier League , Arsenal  London ina  kibarua   dhidi  ya  Crystal Palece leo jioni (10.04.2017) na  mtihani  mkubwa  kwa  kocha  wao  Aserne Wenger wakati  timu  hiyo  iliyoko  katika  nafasi  ya  6  na pointi 54  ikiwania  kurejea  katika  timu  bora  nne  na kufuzu  kucheza  katika  Champions League  msimu  ujao. Mafanikio  ya  Arsenal  leo  yatatuliza  mzuka  wa mashabiki  ambao  wanataka  kocha  huyo  aachie  ngazi baada  ya  kupata matokeo  yasiyoridhisha  msimu  huu katika  ligi  ya  nyumbani  na  pia  michuano  ya  kimataifa.

England Premier League Ronald Koeman
Kocha wa Everton Ronald Koeman Picha: picture-alliance/Zumapress/D. Klein

Jana  Jumapili (09.04.2017)Everton  ilichafua rekodi  ya  kocha  Craig Schakespeare  wa  Leicester City  kwa  kuirarua  timu  hiyo kwa  mabao 4-2. Leicester  ilishinda  michezo  mitano mfululizo  ya  ligi   baada  ya  kumfuta  kazi  kocha aliyeitawaza  timu  hiyo  bingwa  wa  Premier League  kwa mara  ya  kwanza  katika  historia  ya  klabu  hiyo ,  Februari  mwaka  huu  kufuatia  matokeo mabaya  ambayo  yaliiweka  timu  hiyo karibu  na  kushuka daraja.

Fußball Leicester City  Spieler Riyad Mahrez
Mchezaji wa Leicester City Riyad MahrezPicha: Getty Images/J. Finney

Sunderland  ilishindwa  kuhimili  vishindo  vya  Manchester United  kwa  kukubali  mabao 3-0, Chelsea  ikaimarisha nafasi  yake  ya  uongozi   kwa  ushindi  wa  mabao 3-1 dhidi  ya  Bournemouth. Man City  ikapata  ushindi  wa mabao 3-1  dhidi  ya  Hull City  na  Liverpool  ikaimarisha nafasi  yake  ya  kucheza  michuano  ya  Champions League msimu  ujao  kwa  ushindi  wa  mabao 2-1 dhidi  ya Stoke City.

La Liga

Real Madrid inakaribia  kutawazwa  mabingwa  wa  La  Liga kwa  mara  ya  kwanza   katika  muda  wa  miaka  mitano baada  ya  kutoka  sare ya  bao 1-1  na  Atletico Madrid. Barcelona  ilishangazwa  na  kipigo  cha  kushitua   dhidi ya  Malaga  kwa  mabao  2-0  na  pia  kadi  nyekundu kwa nyota  wao  Neymar.

UEFA Champions League - FC Barcelona vs. Paris Saint-Germain
FC Barcelona , Suarez na MessiPicha: Getty Images/L. Griffiths

Edson Cavani  alipachika  wavuni  mabao 2  na kutengeneza  bao  moja  lingine  wakati  Paris Saint- Germain ikipata  ushindi  wa  mabao 4-0  dhidi  ya Guingmp  na  kuendelea  na  mbio  za  kuifukuzia  Monaco katika  ubingwa   wa   ligi  ya  Ufaransa .

Nice  ambayo  inatengana  na  PSG  kwa  pointi  moja ikiwa  katika  nafasi ya  tatu  ilipata  ushini  wa  mabo  2-1 dhidi  ya  Lille  siku  ya  Ijumaa  , wakati  bao  la  Radamel Falcao  liliipa  ushindi  Monaco  wa  bao 1-0  dhidi  ya Angers siku  ya  Jumamosi.

Ligi  ya  mabingwa  barani  Ulaya , Champions  League inaingia  katika  hatua  yake  ya  robo  fainali  kesho Jumanne  na  Jumatano  katika  mkondo  wa  kwanza , ambapo  Borussia  Dortmund  ya  Ujerumani  inaikaribisha Monaco  ya  Ufaransa  katika  uwanja  wa  Signal Iduna Park mjini  Dortmund, na  ni  timu  hizi zinazoelezwa  kuwa viwanda  vya  vijana  chipukizi  wanaotengenezwa  kuwa nyota  barani  Ulaya.

Champions League 2016/17 5. Spieltag AS Monaco and Tottenham Hotspur FC
Djibril Sidibe wa Monacob akishangilia baoPicha: Getty Images/AFP/V. Hache

FC Barcelona  nao watakuwa  uwanjani  kesho , wakipambana  na  Juventus  Turin  ikiwa  ni  pambano linaloonekana  kuwa  marudio  ya  fainali  ya  msimu  wa mwaka 2014 / 2015.

Kwa  upande  wa  michuano  ya  kombe  la  shirikisho barani  Afrika  klabu  ya  soka  ya  Tanzania   Young Africans   ilifanikiwa  kuiangusha Mouloudia  Alger  ya Algeria    kwa  bao 1-0  jana  Jumapili ,  wakati  TP Mazembe  ya  Jamhuri  ya  kidemokrasi  ya  Congo iliiangusha  JS Kabylie  ya  Algeria  kwa  mabao  2-0. Enugu Rangers  ya  Nigeria  itatoka  sare  ya  mabao  2-2 na  Zesco Utd  ya  Zambia.  KCCA  ya  Uganda ikaiangusha  Al Maery  ya  Misri kwa  bao 1-0 .  Rivers United  ya  Nigeria  itapambana  na  Rayon  Sport  ya Rwanda   Aprili 15.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / APE

Mhariri:Iddi Ssessanga