Armin Laschet: Mgombea ukansela wa CDU | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.08.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Armin Laschet: Mgombea ukansela wa CDU

Waziri Mkuu wa jimbo lenye wakaazi wengi zaidi nchini Ujerumani anaongoza kampeni ya muungano wa wahafidhina katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Akifanikiwa atamrithi kansela Angela Merkel.

Ukiwauliza wapigakura wa kawaida nchini Ujerumani, au wadadisi mashuhuri wa kisiasa mjini Berlin, nani ana nafasi kubwa ya kumrithi Kansela Angela Merkel baada ya uchaguzi wa bunge mwezi Septemba, wengi wao watakuambia (baadhi wakivuta pumzi kubwa): Armin Laschet.

Kama Angela Merkel, Laschet ni mwanachama wa chama cha kifahidhina cha Christian Democratic Union (CDU), ambacho ndiyo chama kikubwa zaidi katika bunge la Ujerumani, Bundestag. Hii ndiyo sababu inayomfanya Laschet mwenye umri wa miaka 60 kuwa katika nafasi ya uongozi. Alau, hilo liko hivyo,  kinadharia.

Armin Laschet ndiye waziri mkuu wa jimbo lenye wakaazi wengi zaidi nchini Ujerumani, la North Rhine-Westaphalia (NRW). Hali ambayo inaweza kumuwekea mazingira mazuri ya kufanikisha azma yake ya kuwa kiongozi mkuu ajaye wa Ujerumani. Na kila kitu kilikuwa kinakwenda vyema kwa kambi ya Laschet.

Soma pia: Maoni: Manifesto ya CDU/CSU haina majibu yanayotosheleza

Mambo yalikuwa hivyo hadi katikati mwa mwezi Julai, lilipzuka janga la mafuriko mabaya yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya 180 katika jimbo la Rhineland-Palatinate na jimbo la Laschet la North Rhine-Westphalia. Tangu wakati huo, amekuwa akikabiliwa na shinikizo na kampeni yake imeyumba.

Wakati wa ziara ya pamoja katika mji wa Erfstadt ulioko kusini-magharibi mwa Cologne, rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alielezea kwa hisia mshtuko wake na wasiwasi mkubwa kwa wenyeji, ambao wengi wao walipoteza kila kitu.

Wakati huo huo, nyuma yake, timu za wapigapicha zilikuwa zinachukuwa picha za Armin Laschet akionekana kutaniana na baadhi ya maafisa wa mji huo. Aliomba radhi haraka kwa tabia hiyo isiyofaa -- ombi ambalo amelirudia mara kadhaa katika siku zinazofuata.

Lakini baada ya hapo, kulikuwepo na ghadhabu zaidi kuhusu ukubwa na athari za mafuriko. "Hatutaanza kubadilisha mkakati wetu wote," alisema Laschet, "kwa sababu tu ya siku kama hii." Matamshi hayo hayakupokelewa vyema hata kidogo katika wakati ambapo watu wengi walikuwa tayari wanazungumzia uwezekano wa kiunganishi kati ya matukio ya hali mbaya ya hewa, kama mafuriko ya kustajabisha nchini Ujerumani na ongezeko la joto la Dunia.

Soma pia: Armin Laschet: Kwa Urusi 'unapaswa kuzungumza zaidi, siyo kidogo'

Mabadiliko yalikuja siku kadhaa baadae: "Sote, alisema, "tunahitaji kufanya tunachoweza kufanya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi."

Bahati mbaya kwa Laschet, hili linaendana na taswira ambayo waangalizi wengi wanayo kumhusu: kuliko kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, hisia ni kwamba kuna upunguzaji mwingi tu na mabadiliko kuhusu ahadi za kisera. Nini, wengi wanajiuliza, anasimamia hasa mgombea huyo?

Aliwahimiza pia wafuasi wake kuangalia mbali ya mzozo wa janga la virusi vya corona: "Mizozo barani Ulaya itaongezka baada ya janga," alisema. "Wakati baadhi ya mataifa yatatoka kwa urahisi, mengi hayataweza. Na kuzingatia hili, ndiyo jukumu." Na hata aliibua umuhimu wa kulinda mazingira -- jambo la kulitilia mkazo kwa waziri mkuu wa jambo ambalo linategemea pakubwa sekta ya makaa ya mawe.

Mapambano magumu

Wakati Laschet alipochaguliwa kama mwenyekiti wa chama mwezi Januari, wengi walimuona kama muungaji mkono mkubwa wa mwelekeo wa Merkel. Wakili huyo wa zamani na mwandishi habari - moja wa manaibu mwenyekiti watano wa CDU tangu 2012 - ameonekana kwa muda mrefu kama mtu wa karibu wa Merkel, pamoja na mrtihi wake wa muda mfupi katika nafasi ya mwenyekiti, Annagret Kramp-Karrenbauer (2018 - 2020).

Soma pia: Warithi watarajiwa wa Merkel watofautiana kuhusu China, Urusi

Ili kupata imani ya chama chake, Laschet aililaazimishwa kuvishawishi vyama vya CDU na CSU kwamba katika kipindi cha muda mrefu aliwakilisha chaguo salaama, bila kujali matokeo ya uchunguzi wa maoni. Alizungumzia uzoefu wake wa miongo kadhaa, na uwaziri mkuu wa jimbo la North Rhine-Westaphalia tangu 2017 - kama mamlaka kubwa kivyake, kwa sababu jimbo hilo ndiyo nyumbani kwa karibu robo ya wakazi wote wa Ujerumani.

"Waziri mkuu wa jimbo ambaye anaeongoza kwa ufanisi jimbo la watu milioni 18 anaweza kuwa kansela," kama anavyopenda kusema.

Kama Merkel, Laschet anaamini katika CDU ya mrengo imara wa kati. "Tutashinda tu iwapo tutabakia imara katikati," ni kauli inayojitokeza mara nyingi katika hotuba zake.

Wakati huo huo, mkatoliki huyo kutoka mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Aachen, huzungumzia mara kwa mara mizizi yake ya Rhineland. Kama ilivyotokea, ni mmoja tu kati ya makansela nane wa Ujerumani ndiyo ametokea North Rhine-Westphalia: Konrad Adenauer, wa kwanza kabisaa, katika zama za baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, alieongoza kuanzia 1949 hadi 1963.

Laschet vs. Soeder

Laschet alipata haki ya kuwa mgombea wa muungano wa wahafidhina kwa nafasi ya kansela kwa kumshinda Markus Soeder, kiongozi wa chama cha Christian Social Unioni (CSU), ambacho ni tawi la Bavaria la muungano wa kihafidhina kilichotoa mchango muhimu katika siasa za Ujerumani katika kipindi cha baada ya vita.

Soeder inajitanabahisha kama mtu wa nyakati zote, mwenye kutazama mbele, hata mwenye haiba. Wakosoaji wake wanakiita kufuata upepo. Ukweli ni kwamba: katika uchunguzi wa maoni, waziri mkuu huyo wa jimbo la Bavaria yuko mbali kabisaa ya Laschet. Wafuasi wa Lascht wanajibu hata hivyo kwa kusisitita kwamba mtu wao ndiyo mpambanaji. Yote inategemea msimamo wa kati

Kujitenga na Merkel

Armin Laschet na Angela Merkel wana rekodi ndefu ya kufanya kazi pamoja: Wakati Merkel alipokabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wanachama wa chama chake kuhusiana na sera yake ya kuwakaribisha mamia kwa maelfu ya wakimbizi tangu 2015, Laschet alibakia kuwa mshirika mtiifu kwake.

Lakini kufuatia makosa na udhaifu katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona, Laschet amejitenga taratibu na kansela.

 

Laschet, Kijani na FDP

Iwapo anataka kuwa kansela, Laschet laazima aviunganishe vyama vilivyokata tamaa vya kihafidhina na kupambana dhidi ya watetezi wa mazingira wanaojiamini. Utafiti wa karibuni unaonseha watetezi hao wa mahzingira wanawakaribia wanahafidhina - Chama hicho cha Kijani hivi sasa kinakadiriwa kuwa chama cha pili kwa ukubwa katika bunge la Ujerumani, Bundestag.

Lakini pia ni mtu amabye anaweza kuunda muungano mwepesi na chama cha Kijani baada ya Septemba. Laschet na chama cha Kijani wana historia ndefu: Baada ya kuingia katika Bundestag mwaka 1994, Laschet alisaidia haraka kujenga uhusiano kati ya chama chake cha CDU na chama cha Kijani.

Laschet amesema mshirika anaempedelea kuunda muungano angekuwa chama cha kiliberali cha FDP. Na kweli Laschet anaongoza muungano kama huo katika jimbo lake la nyumbani.

Kiongozi wa Ulaya

Laschet pia ana uzoefu zaidi wa kisiasa kuliko aliokuwa na Merkel kabla ya kuwa kansela. Mbali ya historia yake ya sheria na uandishi habari, amechaguliwa kwa ngazi za manispaa na shirikisho, na hata katika bunge la Ulaya.

Deutschland Unwetter Steinmeier und Laschet in Erftstadt

RAis wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akiwafariji waathirika wa mafuriko mjini Erftstadt akiwa na kiongozi wa CDU Armin Laschet.

Soma pia: CDU-CSU wazinduwa ilani ya uchaguzi wa Septemba

Na kukulia kwake kwenye eneo la mpaka na Ubelgiji, kunamfanya awe raia wa kweli wa Ulaya. Ana mizizi ya kifamilia nchini Ubelgiji na anazungumza Kifaransa kwa ufasaha. Tangu mwaka 2019, Laschet amaekuwa mwakilishi wa Ujerumani kwa jaili ya uhusiano wa kitamaduni kati ya Ufaransa an Ujerumani na amebakisha uhusiano wa muda mrefu na uongozi wa kisiasa mjini Paris.

Kuhusu uhusiano wa mataifa ya kanda ya Atlantiki, Laschet ana kazi ya kufanya, inagwa alitumia siku kadhaa akitalii nchini Marekani mwaka 2019 katika wadhifa wake wa karibuni kama waziri mkuu w ajimbo. Anapanga kuongeza msukumo wa ushirikiano zaidi na Marekani kuhusu sera za tabianchi na biashara.

Wigo mpana

"Armin Laschet ni mwanasiasa mwenyse vigezo vyote vya kushika wadhifa juu zaidi wa chama na serikali, ikiwemo kwa ngazi ya kitaifa." Hiyo ni kulingana na wavuti ya wakfu unaoshirikiana na CDU wa Konrad Adenauer. Hata hivyo, inaonekana Laschet bado inahitaji kuwashawishi wapiga kura juu ya hili.

Na hata katika safu yake mwenyewe, mgombea huyo bado ana kazi kubwa ya kufanya. Anahitaji kuwashawishi wahafidhina ndani ya chama chake — na vile vile wanachama wanawake, ambao wamekuwa wakijivunia Merkel na bado sasa wanaunda tu karibu robo ya wagombea nchi nzima.

Njia ya kuelekea ukansela bado ni ndefu na yenye vizingiti vingi kwa Laschet.