1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ariel Sharon - Afariki dunia

11 Januari 2014

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon amefariki dunia (Jumamosi 11.01.2014) katika hospitali moja karibu na mji wa Tel Aviv akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa katika hali ya kupoteza fahamu kwa miaka minane.

https://p.dw.com/p/1Ap5O
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon.
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon.Picha: Menahem Kahana/AFP/Getty Images

Sharon amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Sheba akiwa hana fahamu tokea Januari 4 mwaka 2006 baada ya kupata kiharusi.Hali yake ghafla ilizidi kuwa mbaya hapo tarehe Mosi Januari mwaka wakati mafigo yake yalipopata matatizo baada ya kufanyiwa upasuaji.

Ariel Sharon , ambaye alifahamika pia kwa jina la utani kama Arik, alitambulika mara kwa mara pia kama tai, farasi wa vita ama mtu mwenye msimamo mkali. Katika kichwa cha habari cha kitabu cha maisha yake kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza alielezwa kama "Mpiganaji". Katika kila hali hata hivyo alionekana kukubalika na pia kushangaza ama mtu asiyekubaliana na wengine na hata mtu mwenye hisia za chuki. Kwa Waisrael wengi alikuwa "shujaa wa vita vya Youm Kippur". Kwa Wapalestina wengi alikuwa pamoja na kiongozi wa wanamgambo ya Lebanon , "muuwaji wa Sabra na Shatilla.

Asili yake

Sharon alizaliwa karibu na mji wa Tel Aviv mnamo mwaka 1928 akitambulika kama Ariel Scheinermann. Wazazi wake walikuwa Wayahudi waliotokea Ulaya ya mashariki, ambapo walibadilisha jina la ukoo wao na kuwa Sharon-Tal. Maisha ya Sharon yamefungamana kwa karibu sana na historia ya taifa la Israel. Katika vita vya ukombozi mwaka 1948 alipambana kama kiongozi wa kombania ya jeshi la miguu dhidi ya majeshi ya Waarabu. Mwaka 1953 alijenga umoja maalum wa mapambano ya kulipiza kisasi kutokana na mashambulio ya wapiganaji wa Kipalestina. Katika vita vya Youm Kippur mwaka 1973 alianzisha mashambulio ambayo hayakuidhinishwa , alivuka mfereji wa Suez akiwa na jeshi lake lililokuwa na vifaru na kuingia Misri na kisha kupata ushindi.

Meja Generali Ariel Sharon wakati wa Vita vya Siku Sita Mashariki ya Kati. (29.05.1967).
Meja Generali Ariel Sharon wakati wa Vita vya Siku Sita Mashariki ya Kati. (29.05.1967).Picha: picture-alliance/dpa

Harakati zake

Ni wanasiasa wangapi wa ngazi ya juu wa Israel aliowatumia Sharon kupanda katika ngazi ya kisiasa. Amefanikisha kukiingiza chama cha kihafidhina cha Likud katika bunge na akawa na wadhifa wa waziri wa kilimo. Pamoja na hayo alianzisha idara maalum ya usalama.

Wanajeshi wa Israel katika Vita vya Yom Kippur. (08.10. 1973).
Wanajeshi wa Israel katika Vita vya Yom Kippur. (08.10. 1973).Picha: GPO/Getty Images

Katika wakati huo kulikuwa na mashambulio kadha ndani ya Lebanon. Lengo likiwa kukiondoa chama cha ukombozi wa Palestina PLO kutoka katika nchi hiyo jirani iliyoko upande wa kaskazini. Wanamgambo wa Kikristo waliokuwa wakiunga mkono Israel nchini Lebanon walisaidia mapambano dhidi ya PLO katika kambi ya wakimbizi ya Sabra na Shatilla mjini Beirut. Wanamgambo waliwauwa mamia ya Wapalestina. Mauji hayo , yaliyofanyika katika eneo linalodhibitiwa na Israel , yalizusha malalamiko makubwa kimataifa.

Tume ya uchunguzi ya Israel ilimpata Sharon na hatia ya kushiriki katika umwagikaji huo mkubwa wa damu. Mwaka 1983 alijiuzulu wadhifa wa waziri wa ulinzi, na akabaki kuwa waziri asiye na wizara maalum katika baraza la mawaziri. Nchini Ubelgiji ukaazishwa uchunguzi wa kesi dhidi ya Sharon kutokana na matumizi ya nguvu aliyoyaongoza, lakini uchunguzi huo haukuendelea. Mfumo wa sheria wa Ubelgiji ulikuwa katika wakati huo kwamba mashataka kama hayo yaliwezekana kupitia kile kinachotambulika kama msingi wa sheria wa dunia.

Haiba yake

Hata hivyo hali hiyo haikuathiri heba yake kisiasa. Sharon alishika nyadhifa katika miaka iliyofuata ya waziri wa mambo ya kigeni, biashara na waziri wa ujenzi. Mwaka 2001 alichaguliwa kuwa waziri mkuu. Alitangaza kujiuzulu mwaka 2005 kutoka wadhifa wa waziri mkuu Kutokana na mvutano wa ndani wa kisiasa katika chama na kujitoa kutoka chama cha Likud na kuunda chama kipya cha Kadima.

Ariel Sharon akigusa Ukuta Mtakatifu Jerusalem. (07.02.2001) .
Ariel Sharon akigusa Ukuta Mtakatifu Jerusalem. (07.02.2001) .Picha: AP

Dhidi ya Wapalestina Sharon alijionesha kwa muda mrefu kuwa ni mtu mwenye msimamo mkali bila kiasi. Usalama wa Israel ulikuwa mbele zaidi kuliko lengo lake kuu.

Sharon pia alikuwa anapenda kuchochea mambo. Alianzisha ujenzi wa nyumba katika eneo la Waarabu katika mji wa kale wa Jerusalem. Mwezi Septemba 2000 alisababisha kuzuka kwa ghasia na maandamano pale alipofanya ziara katika eneo takatifu kwa Waislamu mjini Jerusalem na kuzusha hali mpya ya wasi wasi. Mauaji yaliyotokana na ghasia hizo yalizusha kile kinachofahamika na Wapalestina kama Intifada ya pili.

Mapambano haya ya Wapalestina walidumu kwa muda wa miaka minne.

Ariel Sharon katika mojawapo ya mikutano ya mawaziri ofisini kwake Jerusalem. (10.10.2005.)
Ariel Sharon katika mojawapo ya mikutano ya mawaziri ofisini kwake Jerusalem. (10.10.2005.)Picha: Gali Tibbon/AFP/Getty Images

Sharon alijiweka kando baadaye na msimamo wake mkali. Tai huyu aliyaondoa majeshi ya Israel kutoka ukanda wa Gaza na makaazi ya Wayahudi aliyaondoa kutoka eneo hilo. Katika kitabu chake cha maisha yake amesisitiza kuwa Wayahudi na Waarabu wanaweza kuishi pamoja. Kwa tathimini ya balozi wa zamani wa Israel nchini Ujerumani Avi Primor waziri huyo mkuu wa zamani aliendelea kubaki na msimamo wake huo. Ariel Sharon hakubadilisha nadharia yake, ama msimamo wake kisiasa na hata silika yake haikubadilika, ameandika Primor katika jarida la "Cicero".

Sharon amekuwa mara nyingi mtu wa kutambua hali halisi inayobadilika ambayo huikubali katika hali yake.

Januari 4 mwaka 2006 waziri huyo mkuu alipata mshituko wa moyo. Tangu wakati huo amekuwa katika hali ya kuzimia.

Mwandishi : Giorzewski, Adreas (Nahost-Autor) / zr / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohamed Dahman