Argentina yabeba Copa America kwa kuibwaga Brazil | Michezo | DW | 12.07.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Argentina yabeba Copa America kwa kuibwaga Brazil

Matukio mawili ya ukame wa muda mrefu yalifikia kikomo Jumamosi katika fainali ya Kombe la Amerika Kusini. Argentina ilishinda taji lake la kwanza kuu tangu mwaka wa 1993 baada ya ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Brazil

Na Lionel Messi hatimaye alinyanyua kombe lake la kwanza kuu akiwa na timu yake ya taifa na kujaza mojawapo ya mapengo makubwa kabisa katika taaluma yake yenye mafanikio makubwa.

Bao la ushindi ls Argentina katika dimba la kihistoria la Maracana mjini Rio de Janeiro lilikuja katika dakika ya 22 kutoka kwa Angel di Maria mwenye umri wa miaka 33.

Na baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, Messi mwenye umri wa miaka 34 alilia machozi ya furaha. Baada ya kupoteza mara nne katika fainali, kuondolewa mapema katika mashindano makubwa na hata uamuzi wa kustaafu soka la timu ya taifa, nyota huyo alisherehekea kwa aina yake. Messi alikuwa na umri wa miaka 6 wakati Argentina ilishinda kombe mara ya mwisho. Katika mashindano haya ya Copa America, ametajwa kuwa mchezaji bora akiwa na mabao manne na asisti tano. Nahodha huyo pia alivunja rekodi ya kuichezea timu ya taifa, mechi 151.

AFP, AP, Reuters, DPA