1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arab League yakutana kuhusu giza la Gaza

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvRF

CAIRO:

Maofisa wa jumuia ya nchi za Kiarabu la Arab League- wamekutana kwa mkutano wa dharura kujadilia mzingiro wa Israel kwa ukanda wa Gaza ambao umesababisha kufungwa kwa mtambo pekee wa nguvu za umeme. Hali hii inatishia kuzuka kwa mgogoro wa kiutu.

Wajumbe wa kudumu wa jumuia hiyo wa watu 22 wanakutana kuiomba jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel kuondoa mzingoro huo kwa Gaza. Mtambo pekee wa nguvu za umeme wa Gaza ulifungwa jana jumapili kutokna na ukosefu wa mafuta na hivyo kuliweka eneo hilo katika giza .Lakini yeye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel - Arieh Mekel- amesema kuwa mzingiro utaendelea.

Ukanda wa Gaza,ambako wakazi wake wanaofikia millioni moja Unusu wanategemea msaada,umekuwa chini ya mzingiro wa Israel tangu Alahamisi ya wiki jana pale Israel ilipofunga mipaka yake na eneo hilo kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya maroketi kutoka Gaza.