APR ya Rwanda-mabingwa wa Kagame Cup | Michezo | DW | 22.01.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

APR ya Rwanda-mabingwa wa Kagame Cup

Mabingwa wapya wa Kombe la CECAFA la Afrika Mashariki na Kati ni APR-timu ya wanajeshi ya Rwanda.APR iliizaba Revenue Authority ya Uganda 2:0 na jkulibakisha kombe la kagame nyumbani Kigali.

APR-timu ya majeshi ya Rwanda, ni mabingwa wapya wa Kombe la Kagame ,Sepp Blatter,rais wa FIFA amuungamkono Michel Platini dhidi ya Lennert Johansen kuwa rais mpya wa UEFA ijumaa hii mjini Düsseldorf.

Manchester United, yafungua bado mwanya wa pointi 6 katika Premier League-licha ya kuzabwa mabao 2-1 na Arsenal.Na mzaliwa wa Kenya Moshir salim Jawhar-zamani Stephen Mucheru arudishiwa uraia wake wa Bahrein baada ya kuomba radhi.

APR ya Ruwanda imeibuka mabingwa wapya wa Kombe hilo baada ya jumamosi kuizaba Revenue Authority ya Uganda mabao 2:0 na kutoroka na kombe lao la Kagame na kitita cha dala 30.000 mjini Kigali.

Katika premier League-ligi ya Uingereza,Manchester united ilipewa darasa mwishoni mwa wiki na Arsenal London i,lipozabwa mabao 2:1.Hatahivyo, inaongoza bado ngazi ya Ligi ya uingereza ikiwa imefungua bao mwanya wa pointi 6.Mabao ya dakika za mwisho ya Robin van Persie na Thierry Henry,yameipatia pointi 3 Arsenal licha ya kwamba ilikua Wayne Rooney alieufumania kwanza mlango wao.Chelsea walilazwa mabao 2:0 na Liverpool.

Katika Serie A, Ligi ya Itali, Inter Milan imepanua zaidi uongozi wake kileleni hadi pointi 11 kwa kuikumta Fiorentina mabao 3-1.

Katika La Liga- ligi ya Spain, FC barcelona, mabingwa wamerudi kileleni mkufuatia Sevilla kumudu sare tu ya 0:0 na Villarreal.Barcelona iliizaba Tarragopna mabao 3-0.

Hata katika Ligi ya Holland, PSV Eindhoven wanaongoza kwa mwanya wa pointi 11 kileleni .Hii inafuatia ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Heerenveen.

Rais wa UEFA –shirikisho la dimba la Ulaya, atachaguliwa upya ijumaa ijayo katika kikao maalumu mjini Düsseldorf, Ujerumani.Rais wa sasa ni Mswede Lennert Johanssen ambae wakati mmoja alitoa changamoto klubwa kwa rais wa FIFA Sepp Blatter akitaka kuwa rais wa FIFA.

Si ajabu Blatter amuungamkono Michel Platini, aliekua nahodha wa Ufaransa kuwa rais mpya wa UEFA na sio Johanssen, aliedhibiti kiti hicho cha UEFA tangu miaka 16 iliopita.

Blatter anadai kwamba, tangu 1998 pale kombe la dunia lilipöochezwa Ufaransa, Platini amekuwa mshirika wake mkubwa.

Kombe la dunia la handball linaendelea wakati huu nchini Ujerumani.Mabingwa Spain,wenyeji Ujerumani na mabingwa wa olimpik -Croatia ni miongoni mwa timu 8 zilizokata tiketi zao kwa duru ijayo.Katika kundi A, Tunisia na slovenia pia zimesionga mbele na kuingia duru hiyo.

 • Tarehe 22.01.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcn
 • Tarehe 22.01.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcn