ANKARA.Uturuki yapewa hadi Desemba kurekebisha uhusiano wake na Cyprus | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA.Uturuki yapewa hadi Desemba kurekebisha uhusiano wake na Cyprus

Umoja wa nchi za Ulaya umeipa Uturuki hadi mwezi ujao wa Desemba kurekebisha uhusiano wake na Cyprus na kufahamisha kwamba hiyo ndio nafasi ya mwisho kwa nchi hiyo ya kuokoa juhudi zake za kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Waziri mkuu wa Finland Matti Vanhanen ambae nchi yake ndio inashikilia urais wa umoja wa ulaya amesema mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa umoja huo watatoa uamuzi juu ya uanachama wa Uturuki katika mkutano wao wa Desemba 11 mjini Brussels nchini Ubelgiji lakini itategemea iwapo Uturuki itakuwa imefuata agizo la kufungua tena bandari zake kwa meli za eneo la Cyprus linalotawaliwa na wenye asili ya Ugiriki.

Vanhanen ameonya kuwa iwapo Uturuki haitakuwa imetekeleza agizo la nchi za umoja wa ulaya basi tegemeo lake la kuwa mwanachama wa umoja huo huenda likazama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com