Ankara.Ndege yaanguka ikiwa katika majaribio na kumuuwa rubani wake. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara.Ndege yaanguka ikiwa katika majaribio na kumuuwa rubani wake.

Ndege ya Uturuki aina ya Jet F-16 ikiwa katika majaribio ya kuruka kusini mashariki mwa nchi hiyo imeanguka na kumuua rubani pekee aliyekuwemo katika ndege hiyo.

Akizungumza na shirika la habari la Anatolia Gavana Mevlut Atbas, wamesema mabaki ya ndege hiyo yalikutikana kwenye maeneo ya milima katika jimbo la Bitlis.

Chanzo hasa cha ajali hiyo hadi hivi sasa bado hakijafahamika.

Ndege hiyo iliruka kutoka kituo cha kijeshi karibu na Diyarbakir, ambako ndio sehemu kuu ya Wakurdi kusini mashariki, ambako jeshi kwa hivi sasa limejiimarisha zaidi ili kupambana na waasi wa ki-Kurdi wanaotaka kujitenga.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com