ANKARA:Majeshi ya Uturuki yanaendeleza juhudi ya kuwasaka waasi wa PKK | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA:Majeshi ya Uturuki yanaendeleza juhudi ya kuwasaka waasi wa PKK

Majeshi ya Uturuki bado yanaendelea na operesheni ya kuwasaka waasi wa Kikurdi karibu na milima ya maeneo ya mpakani na Irak.

Helikopta za jeshi la Uturuki zimeshambulia maeneo yanayoaminiwa kuwa ni ya waasi wa Kikurdi katika jimbo la Sirnak kusini mashariki mwa Uturuki.

Wanajeshi wanne wa Uturuki wameuwawa katika mapigano ya siku mbili zilizopita dhidi ya waasi hao wa PKK.

Kiongozi wa KIkurdi Massud Barzani amesema kuwa hatapokea amri kutoka Uturuki inayomtaka kuwasaka na kuwamaliza waasi wa Kikurdi wanaojificha katika jimbo lake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com