ANKARA:Majeshi ya Uturuki yameshambulia vituo kadhaa vya waasi wa Kikurdi | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA:Majeshi ya Uturuki yameshambulia vituo kadhaa vya waasi wa Kikurdi

Majeshi ya Uturuki yameshambulia vituo kadhaa vinavyoshukiwa kuwa ni vya waasi wa Kikurdi katika eneo la kaskazini mwa Irak.

Wapiganaji 34 wa Kikurdi wameripotiwa kuuwawa.

Duru za kijeshi nchini Uturuki zimefahamisha kwamba ndege za kivita ziliingia ndani ya Irak umbali wa kilomita 20 huku takriban wanajeshi wake 300 wa ardhini wakiwa njiani kuelekea katika eneo hilo.

Awali waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alionya kuwa nchi yake haitavumilia kwa muda mrefu kungojea serikali ya Irak iwachukulie hatua waasi hao wa Kikurdi.

Wakati huo huo serikali ya Uturuki pia imeamuru kufungwa ofisi zote za chama cha wafanyakazi wa Kikurdi nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com