ANKARA : Uturuku yashutumu hatua ya Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA : Uturuku yashutumu hatua ya Umoja wa Ulaya

Uturuki leo hii imeshutumu uamuzi wa Umoja wa Ulaya kukawalisha mazungumzo yake ya kujiunga na umoja huo kuwa sio wa haki lakini imeahidi kuendelea na mageuzi kwenda sambamba na kanuni za Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Uturuki wameushutumu umoja huo wa nchi wanachama 25 kukosa dira juu ya dhima ya taifa hilo la Kiislam lisilofungamana rasmi na didi yoyote katika uhusiano wa mataifa ya magharibi na mashariki na wameutaka umoja huo kuweka uzito wake katika kutatua mzozo wa Cyprus ambao ni kiini cha machafuko ya hivi sasa.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayip Erdogan alilihutubia bunge la Uturuki leo hii kuelezea suala hilo.

Uamuzi wa kukawilisha mazungumzo ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya unatazamiwa kuidhinishwa rasmi hapo kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com