1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Gul kuwania tena urais Uturuki

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZS

Chama tawala nchini Uturuki AK kimemteuwa tena Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Abdullah Gul kuwa mgombea wake kuwania uchaguzi wa rais wiki ijayo.

Kuteuliwa kwa Gul hapo mwezi wa April kuwania wadhifa huo kulichochea maandamano makubwa ya umma katika miji mikubwa ya nchi hiyo na kukilazimisha chama cha AK chenye mizizi ya siasa za Kiislam chini ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan kuitisha uchaguzi wa haraka.

Waturuki wanaopinga kufungamanisha dini na taifa wakiwemo magenerali wa kijeshi wenye ushawishi mkubwa nchini humo wanahofu kwamba chama cha AK kinataka kudhoofisha utaratibu huo wa kutenganisha dini na taifa katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya Waislamu jambo ambalo chama hicho inalikanusha.