1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Bunge la Uturuki lamchagua rais mpya

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXQ

Bunge jipya la Uturuki linapiga kura hii leo kumchagua rais mpya wa nchi hiyo. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki, Abdullah Gül, anatarajiwa kushinda, miezi kadhaa tangu wasomi nchini humo walipomzuilia mara ya kwanza alipojaribu kugombea wadhifa huo.

Naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Republican People´s Party, CHP, nchini Uturuki, Onur Oymen, anapinga vikali bwana Gül kugombea wadhifa wa uraisi nchini humo.

´Anajulikana kwa mawazo yake dhidi ya kanuni msingi za taifa letu, kuanzia kutenganisha dini na maswala ya nchi. Mtu wa aina hiyo hapaswi kuwa rais wa Uturuki.´

Uchaguzi wa leo ni raundi ya kwanza kati ya raundi nne na bwana Gül anatarajiwa kuchaguliwa wakati wa kikao cha tatu mnamo tarehe 28 mwezi huu.

Chama chake cha AK kina idadi ya kutosha kuweza kumchagua kuwa rais wa Uturuki licha ya upinzani mkali.