1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel ziarani mjini Kabul

Heinzle / Oummilkheir5 Novemba 2007

Kansela aahidi misaada zaidi kuiwezesha Afghanistan idhamini wenyewe usalama wake hatua baada ya hatua

https://p.dw.com/p/C7fO
Picha: AP

Kansela Angela Merkel amefanya z iara ya ghafla mjini Kabul na kuahidi misaada zaidi katika kuvipatia mafunzo vikosi vya usalama vya Afghanistan.Juhudi za kuimarisha utulivu zinabidi „zijipatie zaidi sura ya kiafghani“-amesema kansela Angela Merkel jumamosi iliyopita,baada ya mazungumzo pamoja na rais Hamid Karsai.

Ziara hiyo ya ghafla ya kansela Angela Merkel imefanyika pakiweko ulinzi mkali.Kansela Angela Merkel hakusafiria ndege ya serikali chapa Airbus ,hasha,ilikua ndege ya kijeshi yenye mitambo ya kinga dhidi ya makombora-Transall ndiyo iliyomsafirisha kansela hadi Kabul.Hakupanda gari,alitumia helikopta kutoka eneo hatari kati ya uwanja wa ndege na kati kati ya mji mkuu Kabul.Ratiba ya ziara yake iliwekwa siri pia kwasababu za usalama.

Mjini Kabul ajenda ya mazungumzo iligubikwa na mada za kisiasa:kwanza pamoja na muakilishi wa Umoja wa mataifa Tom Koenigs,kiongozi mpya wa tume ya Ulaya inayosimamia shughuli za polisi Scholz na mkuu wa vikosi vya kimataifa vinavyosimasmiwa na NATO-ISAF-jenerali McNeill.Kilele cha awamu ya mwanzo ya ziara hiyo yalikua mazungumzo pamoja na rais Hamid Karsai katika kasri linalolindwa vikali mjini Kaboul.

Katika mazungumzo hayo kansela Angela Merkel aliahidi:

„Shirikisho la jamhuri ya Ujerumani litaisaidia Afghanistan kwa moyo mkunjufu na kwa nguvu zake zote.“

Kansela Angela Merkel ameshadidia umuhimu wa kuwaona waafghani wakijibebesha zaidi jukumu la kuijenga upya nchi yao.Lengo la sera ya Ujerumani ni kuiona Afghanistan ikidhamini hatima yake hatua baada ya hatua.Mbali na misaada ya maendeleo,sera hizo ni pamoja na kuimarishwa vikosi vya wanajeshi na kupatiwa ,mafunzo polisi.

Askari polisi 40 wa Ujerumani wanatumikia kikosi cha polisi wa Ulaya EUPOL nchini Afghanistan.Idadi hiyo ni ndogo mno wanahisi wataala pamoja pia na serikali ya Afghanistan mjini Kaboul.

Kansela Merkel pia anasisitiza umuhimu wa kuzidi kupatiwa mafunzo askari polisi.

„Tutaangalia ,kama kuna uwezo wa kuzidisha juhudi hizo –kuambatana na mjadala wa bajeti.Mafunzo ya vikosi vya polisi ni mada muhimu ili wananchi wa Afghanistan waweze kuamini wanaishi katika nchi inayolinda usalama wao.Nnafikiri umefika wakati ambapo juhudi za usalama zitabidi hatua baada ya hatua kuchukua sura ya kiafghanistan.“

Kansela Angela Merkel ameshadidia msimamo wa serikali yake dhidi ya kuwekwa wanajeshi wa Ujerumani katika maeneo ya kusini mwa Afghanistan.Wanajeshi wa Ujerumani wataendelea kuwepo katika maeneo ya kaskazin-amesema kansela kabla ya kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani katika kambi yao kubwa kabisa huko Mazari-Shariff,kaskazini mwa Afghanistan .

Hii ni ziara ya kwanza ya kansela Angela Merkel tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita na ya pili kuwahi kufanywa na kansela wa Ujerumani tangu ziara ya mtangulizi wake Gerhard Schröder october mwaka 2004.