ANC -Mbeki au Zuma ? | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

ANC -Mbeki au Zuma ?

Jacob Zuma aonesha atamshimnda leo rais Thabo Mbeki katika kinyan'ganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa ANC.

default

Rais Thabo Mbeki (kushoto) na Jacob Zuma

ANC-chama-tawala nchini Afrika Kusini,wameanza mapema asubuhi ya leo kumchagua kiongozi wao wa chama huku ishara zote zikionesha rais wa sasa Thabo Mbeki ataangushwa madarakani na makamo-rais na mpinzani wake mkubwa Jacob zuma.

Bw.Zuma ambae kuwasili kwake mkutanoni kulishangiriwa kwa shangwe na wajumbe waliojipanga kuanza kupiga kura akionesha furaha ya matumaini ya ushindi huku akiwapongea mkono wafuasi wake .

Ukurasa wa mbele kabisa wa gazeti maarufu la Afrika kusini-THE STAR-umetangaza „Jukwaa limeandaliwa tayari kukaribisha ushindi wa Bw.Zuma.“

Zuma alikuwa wa kwanza kati ya wajumbe 3,900 wa chama-tawala kutia kura yake sandukuni katika chuo kikuu cha Limpopo,unakofanyika mkutano.

Akiwa ameanza usoni kabisa kuliko watetezi wengine pale ulipoaanza mkutano huu wa siku 5,nafasi za Bw.Zuma kama mtu anaeweza sana kuchaguliwa kukiongoza chama cha ANC zilizidi kunawiri na kuimarika tangu jumapili wakati wa majadiliano motomoto ambamo hadhi za uongozi za rais Thabo Mbeki-mwenyekiti wa sasa wa ANC zilibainika kufifia.

Rais Mbeki alieliongoza dola kubwa la kiuchumi barani afrika tangu 1999,akishika hatamu kutoka kwa mzee Nelson Mandela, akionesha hana furahi jioni ya jana akimuona mpinzani wake Jacob zuma akishangiriwa mno na kupewa mikono n a wajumbe mkutanoni huku wakiimba wimbo maarufu wa chama „Umshini Wam .

Ushindi kwa Jacob Zuma utakamilisha kufufuka kwake kisiasa baada ya kashfa ya kumzika ya tuhuma za rushua na ubakaji ,licha ya kwamba yungali anakabili mashtaka ya rushua na ufisadi.

Kwa jicho la wingi mkubwa kupita kiasi wa chama-tawala cha ANC Bungeni,ushindi wa Bw.Zuma katika uchaguzi huu wa mwenyekiti wa chama utamhakikishia nafasi ya kuja kukikalia kiti cha rais wa Afrika kusini utakapofanyika uchaguzi mkuu 2009.

Hatahivyo, Bw.Zuma anakabiliwa na mashtaka ya kula rushua na baada ya kushindwa kesi yake ya karibuni mahkamani kutaka mlolongo wa hati za kusaka nyumba yake zitangazwe si halali.

Wakati rais Thabo Mbeki bado ana kipindi cha miaka 2 kusalia madarakani kama rais wa Afrika Kusini, kushindwa na Bw.Zuma katika uchaguzi wa leo bila ya shaka kutamvunjia heba yake .Kuna wachambuzi wanaofika umbali wa kudai Mbeki aweza kukabili changamoto za kambi ya Bw.zuma kumtaka an’gatuke hata na mapema.

Wanasiasa hawa wawili-Bw.Thabo Mbeki na Jacob zuma waliteuliwa rasmi hapo jana na chama baada ya patashika kubwa nyuma ya pazia kugombea wadhifa wa urais wa chama.

Uchaguzi ulipangwa kuanza tayari saa 12 alfajiri ya leo ,lakini kulicheleweshwa kwa masaa 3 kutokana na kukawia kuchapishwa karatasi za kura.Hii imesababisha milolongo mirefu ya wajumbe nje ya Maktaba ya chuo kikuu cha Limpopo.

Zuma ameungwamkono na matawi 5 kati ya 9 ya mikoa ya Chama cha ANC.Wajumbe lakini hawalazimiki kufuata mapendekezo ya mkoa.

Akiwa wa asili ya kabila la Zulu,Jacob Zuma amenufaika mno na kuvunjwa moyo mno na rekodi ya serikali ya chama cha ANC kutimiza ahadi zake za kuondoa umasikini katika kipindi chake cha utawala wa miaka 13 tangu kumalzika kwa utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.

 • Tarehe 18.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Cd79
 • Tarehe 18.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Cd79

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com