AMSTERDAM: Polisi wawakamata watu 6 watuhumiwa wa mtandao mpya wa kigaidi wa kiislamu | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMSTERDAM: Polisi wawakamata watu 6 watuhumiwa wa mtandao mpya wa kigaidi wa kiislamu

Polisi nchini Uholanzi wamewakamata watu 6 wanaotuhumiwa kuwajiri watu wa kujitolea katika vita vya jihad. Watuhumiwa hao sita, wanamume watano na mwanamke moja, sasa wametiwa ndani mjini Amsterdam mapema leo asubuhi. Wendeshamashitaka nchini Uholanzi wamesema kukamatwa watu hao ni matokeo ya uchunguzi juu ya mtandao wa kimataifa wa magaidi wa kiislamu ulioanzishwa mwezi Novemba mwaka 2005. Watatu miongoni mwa watuhumiwa hao, walikwenda nchini Azerbaijan katika mafunzo ya vita vya jihad. Walikamatwa huko na kurudishwa nchini Uholanzi. Watuhumiwa hao 6 wanatarajiwa kuhojiwa na jaji baadae wiki hii ambapo itaamuliwa iwapo wasalie ndani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com