AMSTERDAM: Kuelekea kuundwa serikali ya muungano | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMSTERDAM: Kuelekea kuundwa serikali ya muungano

Matokeo ya uchaguzi nchini Uholanzi hayajakamilisha muelekeo wa kisiasa baada ya vyama mashuhuri kushindwa kupata wingi wa viti kuweza kulidhibiti bunge. Chama cha waziri mkuu, Jan Peter Balkenende cha Christian Demokratik, kimeonekana kuwa mshindi kwa kunyakua viti 41juu ya viti 150 vinavyowaniwa katika baraza la wawakilishi. Lakini kutokana na hali kwamba chama kikubwa cha upinzani cha Leba kilipata viti 32 na chama cha Socialist kupanda kutoka viti 9 hadi viti 26, haijaonesha mnamna itakavyoundwa serikali ya mseto. Wadadisi wa maswala ya kisiasa wamesema, kusamabaratisha kura na uungwaji mkono unaozidi kupanda kwa vyama vidogo vidogo vya kisiasa, kutapelekea kurefusha mazungumzo kwa ajili ya uundwaji wa serikali ya muungano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com