1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Wenye silaha Niger wanauwa watoto zaidi

13 Septemba 2021

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema idadi kubwa ya watoto inakabiliwa na hatari ya mashambulizi, machafuko na kusajiliwa na makundi ya wapiganaji nchini Niger.

https://p.dw.com/p/40FGQ
Niger Symbolbild Angriff auf französische Touristen
Picha: AFP/L. Marin

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema idadi inayoongezeka ya watoto wanauwawa au kulengwa kwa ajili ya kusajiliwa katika makundi ya wanamgambo, katika machafuko yanayoendelea katika mpaka wa Niger na Mali na Burkina Faso.

Naibu mkurugenzi wa Amnesty kitengo cha kukabiliana na mizozo Matt Wells amesema makundi ya wanamgambo yamevamia shule mara kwa mara na yanawalenga watoto.

Shirika hilo limeyalaumu makundi ya kigaidi ya Dola la Kiislamu huko Sahara ISGS na kundi lililo na mafungamano na al-Qaeda la Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin JNIM, kwa masaibu yanayowakumba watoto katika eneo hilo.