AMMAN.Rais Bush na waziri mkúu wa Irak Nuri al Maliki kufanya mkutano wao leo | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMMAN.Rais Bush na waziri mkúu wa Irak Nuri al Maliki kufanya mkutano wao leo

Rais George W Bush wa Marekani yupo nchini Jordan ambapo leo atakutana na waziri mkuu wa Irak Nuri al Malik.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika jana baina ya viongozi hao wawili na mwenyeji wao mfalme Abdullah wa Jordan uliahirishwa bila ya kutolewa maelezo yoyote.

Rais Bush na bwana al Maliki watajadili njia za kuleta usalama nchini Irak.

Waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki ameenda nchini Jordan kukutana na rais Bush licha ya upinzani mkali wa jamii za Wasunni na Washia zilizomtaka asifanye ziara hiyo.

Mawaziri wanne wa Kishia pamoja na wabunge 30 wa jumuiya ya Kishia inayoongozwa na Muktada al Sadr mwenye mlengo mkali wamejiuzulu, kupinga mkutano wa waziri mkuu al Maliki na rais Bush nchini Jordan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com