1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN: Jordan yamuunga mkono Rice

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF8

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleza Rice amekuwa na mazungumzo na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan, katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Taarifa iliyotolewa na kasri ya mfalme Abdullah imemtaka Condoleza Rice katika juhudi zake hizo kushirikiana na nchi zote za kiarabu pamoja na jumuiya ya kimataifa.

Imesisitiza kuwa Mfalme Abdullah anaunga mkono juhudi za Marekani katika kufufua mazungumzo hayo kwa pande hizo mbili Israel na Palestina kwanza kukubaliana.

Condeleza Rice aliwasili mjini Amman akitokea Jerusalem katika ziara yake ya eneo hilo ambako alikuwa na mazungumzo na Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas.