1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Washukiwa wawili wa ugaidi wauwawa

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzA

Vyombo vya habari nchini Algeria vimeripoti hii leo kwamba wanajeshi wa Algeria jana waliwaua watu wawili walioshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu mashariki mwa mji mkuu Algiers.

Inadaiwa washukiwa hao walikuwa wakisafiri ndani ya gari wakati waliposimamishwa kwenye kituo cha upekuzi kilichojengwa karibu na kambi ya jeshi la Algeria.

Duru zinasema mtuhumiwa mmoja aliuwawa papo hapo na mwengine akakimbia kabla kufukuzwa na kuuwawa.