Al-Shabaab wauwa 7, wajeruhi 20 Mogadishu | Matukio ya Afrika | DW | 25.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Somalia

Al-Shabaab wauwa 7, wajeruhi 20 Mogadishu

Watu saba wameuwawa na 20 kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabaab kuivamia hoteli moja mjini Mogadishu kwa magari yaliyojaa mabomu.

Polisi  na watu  walioshuhudia  wamesema  leo kwamba  mripuko  wa  kwanza  ulitokea  katika  lori  lililokuwa  limewekwa  miripuko karibu  kabisa  na  sehemu  ya  mbele  ya  hoteli hiyo, wakati  mripuko  wa  pili  ulikuwa  wa  bomu  lililowekwa  ndani  ya  gari iliyokuwa  imeegeshwa  karibu  na  hoteli. 

Wapiganaji  wa  kundi  la  kigaidi  la  al-Shabaab  walivamia  hoteli  hiyo ya  Dayah, ambayo  inatembelewa  zaidi  na wafanyabiashara  na  maafisa  wa  serikali  baada  ya  shambulio  hilo  la  mabomu. 

Afisa  wa  Usalama,  Mohammed Hassan, amesema  idadi  ya  watu  waliouwawa  inatarajiwa  kupanda  kwa sababu  baadhi  ya  watu huenda  wamenaswa ndani ya hoteli hiyo yenye ghorofa  tatu.

Watu  wengine  20  wamejeruhiwa kwa  mujibu  wa  polisi.