Al Qaeda wabadili mbinu | Habari za Ulimwengu | DW | 09.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Al Qaeda wabadili mbinu

---

BAGHDAD

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani nchini Iraq, yamegundua kasha la pili kwa ukubwa la silaha lililowahi kuonekana mjini Baghdad.Hii ilifuatia taarifa waliopewa na kikosi kimoja cha kujitolea.

Katika shehena hiyo na kuna aina mbali mbali ya mabomu ya kuharibu vifaru, mabomu ya mkono pamoja na zana nyingi kabisa za kutengezea miripuko.

Taarifa nyengine kutoka Baghdad , zinasema kwamba mtandao wa Al Qaeda unabadili mbinu zake za kupigana katika jimbo la machafuko la Diyala, nchini Iraq.Hii imefahamika baada ya bomu la kujitoa mhanga kuua watu 8 katika mji huo wenye kinu cha kusafishia mafuta.Taarifa hii ametoa Meja-jamadari Mark Hertling .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com