1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Maliki na wanaomkosoa Marekani

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTF

BAGHDAD:

Waziri mkuu Al Maliki wa Iraq aliekumbana karibuni na misukosuko ya kukosolewa ,amewakaripia wanaomkosa huko Marekani kwamba hawathamini mafanikio iliopata Iraq na hawaelewi jinsi ilivyoshida kujenga nchi upya baada ya miongo kadhaa ya vita na utawala wa kidikteta.

Al maliki akasema baadhi ya tuhuma kutoka Marekani zilizotoka kabla ya ripoti ya mwezi huu wa Septemba hazisaidii kitu.Nouri al Maliki akasema wakosoaji wake nchini Marekani yamkini hawajui kiwanga gani Irak imeteketezwa na hivyo hawathamini mchango mkubwa uliotolewa na serikali ya Iraq na mafanikio yake.