Al Ahly yatamba Dar-es-salaam mbele ya Young Africans. | Michezo | DW | 06.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Al Ahly yatamba Dar-es-salaam mbele ya Young Africans.

Bayern munich yachezeshwa kindum,bwe-ndumbwe na Wolfsburg 5:1.

Wolfsburg's Grafite, akitia bao la ajabu.

Wolfsburg's Grafite, akitia bao la ajabu.

Mabingwa wa Afrika al Ahly ya Misri, wamenguruma mbele ya mabingwa wa Tanzania Young Africans kwa bao 1:0 mjini Dar-es-salaam-

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich, wafedheshwa kwa mabao 5-1 na Wolfsburg-Manchester United yaitandika Aston villa mabao 3-2 na kungangania usukani wa Ligi ya Uingereza.Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika-champions League, Al Ahly ya Misri, wameondoka na ushuindi mwengine mbele ya mabingwa wa Tanzania Young Africans.

Yanga walioahidi kufuta mabao 3 waliochapwa mjini Cairo wiki 2 nyuma, walielemewa dakika ya 5 tu ya mchezo na mwishoewakalazwa kwa bao 1:0 nyumbani mjini Dar-es-salaam .

Pigo la Yaounga, limeirudisha katika ukweli wa mambo baada ya kuota ndoto kufuatia ushindi wao wa duru 2 wa mabao 14 dhidi ya chipukizi Etoile d-Or Mirontsy wa visiwa vya Comoro.

Klabu nyengine za Afrika zilizokata tiketi zao kwa duru ya tatu ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ni :

Kano ya Nigeria, Ahly ya Libya,Merreikh ya Sudan,Contonsport ya Kamerun,Kampala City Copuncil ya Uganda ,TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na hata ZESCO ya Zambia.

TP Mazembe, iliizaba Petro Atletico ya Angola mabao 5-1 wakati ZESCO UTD ya zambia iliikandika Africa Sports ya Ivory Coast 2:0.Canon Yaounde ya kamerun ilitamba nyumbani mbele ya Primieiro Agosto kwa bao 1:0. Al merreikh ya Sudan iliitimua nje Al-Ittihad ya Libya kwa mabao 3:0.

Katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,mabingwa Bayern Munich ,walikiiona Jumamosi kile kilichomtoa kanga manyoya: Katika changamoto ya kuamua wao au Wolfsburg wanachukua usukani kuongoza Ligi, ilikua Wolfsburg iliotamba. Maajabu lakini ni vipi walivyotamba.Sio tu waliikandika Munich mabao 5-1 na kuiabisha,lakini bao la mbrazil Grafeti,alilotia baada ya kuwachenga walinzi 3 na kipa wa Munich,lilikuwa bao la mwaka ambalo daima Bayern Munich halitalisahau.

"Waliocheza kama mabingwa halisi"-alisema Matthias Sammer, mchezaji wa zamani wa taifa na mkurugenzi wa michezo wa Shirikisho la dimba la Ujerumani.

Na gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung likaandika:

"Kulinyakua taji la ubingwa si miujiza tena."

Kwa ushindi huo ,Wolfsburg sasa imeparamia kileleni mwa Bubndesliga na huo ulikuwa ushindi wao 8 mfululizo.Wolfsburg inehujumu kwa mikuki 2-mbrazil Grafeti na Mbosnia Edin Dzeko,kila mmoja alitia mabao 2.

Baada ya kufedheheshwa huko ,kocha wa Bayern Munich ,Jurgen klinsmann alisema:

"Mwishoe, tuliaibishwa.Niliionya timu yangu kuchunga ili mkasa uliotokea miaka 3 iliopita baada ya kutwaa vikombe vyote 2,Munich ikaja kutokea wa4 msimu uliofuatia na kubidi kucheza katika Kombe la UEFA na halafu kutimuliwa kwa kocha wake Felix Magath.Tunataka bado kuibuka mabingwa ,lakini inatupasa kukaa na kzingatia ni nini muhimu kabisa-nacho ni Bundesliga."

Alisema kocha wa mabingwa Bayern Munich.Wiolfsburg sasa inasimama wapi katika ngazi ya Ligi ?Wolfsburg sasa ni viongozi wapya wa Ligi wakiwa na jumla ya pointi 51.

Hamburg pia ina pointi 51 baada ya kuzima vishindo vya Hoffenheim kwa bao 1:0.Hertha Berlin iliokuwa kileleni sasa imeteremshwa baada ya kuzabwa mabao 3-1 nyumbani na Borussia Dortmund.Munich iko nafasi ya 4 ikiwa na pointi 48.

Macho ya mashabviki wa Munich yanakodolewa mpambano wake kati ya wiki hii wa champions League na FC barcelona.Iwapo Munich ikiteleza tena, basi shoka litarudi kumetameta kufyeka kocha Klinsmann.

Jana Werder Bremen, walivunja ubishi wa jirani zao hannover 96 walipiowakomea mabao 4:1.Diego wa Brazil alitia bao la pili lililofanya matokeo 2:1 kabla Claudio Pizarro alipotia bao na kufanya mabao yake msimu huu kuwa 15.

Jana pia Bayer Leverkusen ilijipatia ushimndi mwengine dhidi ya mahasimu wao wa mtaani FC Cologne. Baada ya upinzani mkali,Stefan Kiessling alivunja tumbuu za lango la Cologne kabla stadi wa Cologne wa zamani Helmes kutia bao la 2 kwa mkwaju wa adhabu wa penalty uliochochea hasira uwanjani.Cologne, ilibisha uamuzi wa rifu. Ijumaa Schalke iliikandika Armenia Bielefeld mabao 2-0 wakati Stuttgart ikaichapa Bochum jumamosi mabao 2:1.Frankfurt iliishinda Energie Cotbus mabao 2-1.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza, chipukizi Federico Macheda, akiichezea kwa mara ya kwanza Manchester united ,alilifumania lango la Aston villa kwa bao la ushindi katika dakika za kufidia.Kwa ushindi wa mabao 3-2 jana ,Manu imetoa salamu kwa Liverpool na Chelsea,kwamba ,imeshika uzi wake ule ule wa kutoroka msimu huu na taji la ubingwa.Kwani, Manu sasa ina pointi 68 kutoka mechi 30 na hivyo wako pointi 1 zaidi kuliko Liverpool walioparamia kileleni mwa ligi na mapema hapo Jumamosi walipoitia Fulham.Chelsea, walioshinda New Castle kwa mabao 2:0 hapo Jumamosi,wanajikuta sasa nafasi ya 3 wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 31.