Ajali ya treni na basi yawauwa watu 12 Nairobi | Matukio ya Afrika | DW | 30.10.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ajali ya treni na basi yawauwa watu 12 Nairobi

Kiasi ya watu 12 wameuawa baada ya treni la abiria kuligonga basi lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo mbaya

Mabaki ya basi la abiria lililogongwa na treni jijini Nairobi

Mabaki ya basi la abiria lililogongwa na treni jijini Nairobi

Ajali za barabarani zinazosababisha idadi kubwa ya vifo hutokea kila mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabara na mabasi yanayojaa abiria kupinduka, kila mara huendeshwa kwa mwendo wa kasi na kuyapita magari mengine ili kupata faida ya haraka.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, gari hilo lilikokotwa kwa takribani mita 500 kutoka eneo la ajali. Mkuu wa polisi jijini Nairobi Benson Kibui amesema basi hilo la abiria lilivuka reli wakati treni hilo lilipofika kwa mwendo wa kasi. Ajali hiyo ilitokea wakati wakaazi wengi wa jiji walipokuwa wamejaa barabarani wakielekea makazini saa za asubuhi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri:Josephat Charo