Aichach-Ujerumani:Aliyekua kiongozi wa magaidi wa RAF aachiwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 25.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Aichach-Ujerumani:Aliyekua kiongozi wa magaidi wa RAF aachiwa huru

Kiongozi wa zamani wa kundi la kigaidi la mrengo wa shoto nchini Ujerumani ameachiwa huru. Maafisa wamethibitisha kwamba Brigitte Mohnhaupt aliachiwa huru kutoka gereza la Aichach katika mkoa wa kusini wa Bavaria saa chache zilizopita. Alikua akitumikia vifungo vitano vya maisha kwa kuhusika katika mauaji 9 miongoni mwa yale kadhaa yaliofanywa na kundi hilo lililojiita Jeshi Jekundu. Mwezi uliopita, mahakama mjini Stuttgart iliidhinisha ombi la msamaha lililowasilishwa na Mohnhaupt,ikiamua anaweza kuachiwa huru baada ya kuweko jela kwa miaka 24.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com