1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yakabiliwa na wimbi la 3 la corona

25 Juni 2021

Afrika inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, wakati hospitali zikiendelea kuwapokea wagonjwa na vifo vikishuhudiwa hali ambayo imechangia vituo vya afya kulemewa.

https://p.dw.com/p/3vXbU
Coronavirus Südafrika | Klinik mit Covid-19 Station
Picha: RODGER BOSCH/AFP

Haya yanafanyika wakati ambapo bara hilo likiwa nyuma katika kampeni ya chanjo ya ulimwengu.

Janga la corona limetajwa kuibuka tena kwa kiwango cha kutisha katika nchi zisizopungua 12, huku visa vya maambukizi vikitarajiwa kufikia rekodi ya juu ndani ya wiki tatu.

Mkurugenzi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Afrika CDC, John Nkengasong, ameelezea wimbi la tatu kuwa baya sana.

Hadi kufikia sasa, kirusi cha Delta kilichogunduliwa mara ya kwanza nchini India, kimeripotiwa katika nchi 14 za Afrika.

Idadi kubwa ya maambukizi imeshuhudiwa katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Afrika imeorodhesha maambukizi chini ya milioni 5.3 na vifo ni 139,000.