1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini na kombe la dunia 2010

15 Oktoba 2008

Maandalio yanakwenda barabara miezi 20 kabla firimbi kulia Juni 11.2010.

https://p.dw.com/p/FaCb

Imesalia miezi 20 tu kabla firimbi kulia kuanzisha Kombe la kwanza kabisa la dunia kuchezwa barani Afrika. Wenyeji ni Afrika Kusini, watakaoandaa kombe hilo kati ya Juni 11 hadi Julai 11, 2010 atakapotawazwa bingwa.

Tangu kupewa jukumu hilo, Afrika Kusini,vichwa vya habari visivyopendeza vimekuwa vikitawala.Kwanza kutokana na kuchelewa majenzi ya viwanja na miundo-mbinu kwa jumla: Barabara,mahoteli na usoni kabisa uhalifu uliozagaa nchini.

Ni juzi tu wajumbe 3 mashuhuri wa serikali katika kamati ya Maandalio ya kombe hilo la dunia watiifu kwa rais wa zamani Thabo Mbeki,wameuzuliwa na nafasi yao wameteuliwa wengine.

Hivi sasa lakini ,Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia 2010 chini ya uongozi wa Danny Jordaan,imepata baraka za FIFA -shiriokisho la kabumbu ulimwenguni.Na hata Ujerumani nayo,ilioandaa kombe lililopita la dunia 2006,inaiungamkono Afrika Kusini kwa nguvu zake zote. Inaisaidia katika sekta t ya kijamii na ya utamaduni.

Mapema wiki hii,Kamati ya Maandalio ya Kombe la dunia, ilitoa taarifa katika Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Berlin.

Kwanza wajumbe hao wa kamati ya maandalio walionesha ujenzi unavyoendelea:Iliweza kuonekana viowanja vikiwa nusu vimemalizika katika miji ya cape Town ,Durban ,Johannesberg na vituo vyengine vitakavyochezewa kombe la dunia 2010.Zilikuwa picha zinazomtuliza mtu kuwa kazi inaendelea barabara.Risala unayopata ni kuwa ujenzi unasonga mbele:

Katika filamu ya pili katika Ubalozi huo wa Afrika kusini mjini Berlin, unaona tayari ushabiki na jazba kubwa iliopaliliwa na kombe la dunia .

Hans Klaus ,mkurugenzi wa mawasiliano wa FIFA anaelezea shauku hii kubwa imetoka wapi na kwanini Afrika Kusini imechaguliwa kuandaa kombe hilo la dunia :

"Afrika imetusisimua kwa mchezo wake wa dimba na hata mastadi wake iliotoa.Ni vigumu leo kuiona timu mashuhuri ya ulaya inayocheza bila mastadi wa dimba wa kiafrika."

Na Bw.Horst Schmidt, mshauri wa FIFA kwa kombe la dunia 2010, anaamini kabisa kwamba tutarajie kombe la dunia la shangwe na shamra shamra ambalo litalisisimua bara zima la Afrika.

"Rangi za jazi mbali mbali,ushabiki mkubwa wa mashabiki wa kiafrika uwanjani sio tu utaonekana Afrika Kusini pekee ,bali Afrika nzima.Na hii tangu mwanzo ilikua shabaha ya kwanini Afrika kusini imeomba kuandaa kombe la dunia.Na hii ni zaidi kuliko ilivyokua katika kombe lililopita kuweza pia kulisemea bara zima ."

Danny Jordaan, Mwenyekiti wa kamati ya Maandalio ya kombe hilo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini,hakua na shaka hata sekunde moja kuwa Afrika Kusini itaweza kuandaa mradi huo.Swali halikuwa kukodolewa macho kwa wiki chache tu na walimwengu.

"Ni picha gani za afrika tunataka kuonesha ulimwengu ? Ni picha za bara ambalo linalotatu kwa dhati tatizo la demokrasia,haki za binadamu,elimu na biashara."

Hizo ni shabaha kubwa za kufikiwa ambazo mtu kama Bw.Danny Jordaan, aweza kwa kuaminika kuzipigia upatu.Kiongozi huyu wa maandalio ya kombe la kwanza la dunia baranbi afrika akijiweka upande wa shujaa mkubwa wa Afrika kusini, mzee Nelson Mandela,amejionea jinsi vita vya kukomesha ubaguzi na mtengano vilivyoendeshwa na akiwa kama mbunge alitoa pia mchango wake.

Anakumbusha kwamba Afrika kusini, lilikua taifa lililogawanywa baina ya weupe na weusi.Mtu akahitaji upeo wa kutupa macho mbele na upeo huo ni kombe la dunia 2010 ili kuiwezesha Afrika kusini, kuungana pamoja,kuiimarisha na kusonga mbele kama kitu kimoja.