1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Saumu Mwasimba
15 Julai 2022

Kisa cha kushambuliwa baa moja katika mtaa wa Soweto nchini Afrika Kusini ni moja ya mada zilizoandikwa na wahariri nchini Ujerumani sambamba na simulizi ya mwanariadha Mo Farah kutoka Uingereza.

https://p.dw.com/p/4ECt8
Südafrika | Schüsse in einer Bar in Soweto mit mindestens 15 Toten
Picha: Ihsaan Haffejee/AFP/Getty Images

Frankfurter Allgemeine Zeitung

Mhariri wa gazeti hilo ameandika kuhusu mauaji ya watu 15 yaliyotokana na ufyetuaji risasi katika baa moja huko nchini Afrika Kusini.Mhariri anasimulia jinsi kundi la washambuliaji la wanaume kadhaa lilivyovamia kwenye baa moja ya mtaa wa Soweto wakiwa na bunduki aina ya AK-47 pamoja na bastola na kuanza kuwashambulia ovyo wateja waliokuweko ndani ya baa hiyo. Kwa ujumla watu 21 waliuwawa,katika matukio matatu ya mashambulizi ya ufyetuaji risasi  15 waliuliwa kwenye tukio hilo la Sowetu na 9 wengine walijeruhiwa.Tukio hilo liliripotiwa mwishoni mwa wiki iliyopita.Chama cha upinzani kinachotetea ukombozi wa kiuchumi EFF kimeliita shambulizi hilo kuwa la kigaidi,lakini vyama vingine vya upinzani vimehoji uwezo wa  jeshi la polisi  katika kuzuia mashambulizi ya aina hiyo. Gazet hilo la Frankfurter Algemeine pia limekumbusha kwamba kwa miaka Afrika Kusini imeorodheshwa katika orodha ya takwimu za kimataifa za nchi zenye uhalifu.

die tageszeitung,

Na gazeti la  die Tageszeitung nalo limeitazama Togo,mhariri anasema,ugaidi umeshaingia nchini Togo,mashambulizi ya kutisha yakitikisa kijiji kimoja karibu na mpaka wa BurkinaFaso na kuua watoto tisa. Mhariri anasema kwa mtu kama Dominic Johnson kile hasa kilichotokea bado hakiko wazi ila picha za mwanzo alizozishuhudia ni sawasawa na zile za mauaji ya ukatili yaliyotokea Bucha nchini Ukraine. Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa makundi ya kigaidi walivamia jumapili usiku kijiji hicho cha Togo  na kuwauwa wahanga wao wa mwazo waliokutana nao,watoto tisa waliuliwa kwenye kijiji hicho cha Marba. Mhariri wa die Tageszeitung anaendelea kusimulia kilichotokea kwenye kijiji hicho kwa kuseka kwamba kwanza ulitokea mripuko karibu na shule ya msingi  lakini hakuna aliyeuwawa,dakika 20 baadae  ukatokea mripuko mwingine wa bomu,shambulio hili lililenga kundi la watoto  waliokuwa wakitoka kwenye sherehe za sikukuu ya Eid Al Adha.

Handelsblatt,

Tuligeukie sasa gazeti la Handelsblatt,na mhariri wa gazeti hilo yeye amelitazama zaidi suala la kiuchumi kwa kuilenga Nigeria na utajiri wake wa mafuta.Anasema hakuna nchi ya Afrika yenye hifadhi kubwa ya mafuta kana Nigeria. Hivi karibuni nchi hiyo inaweza kusafirisha  kiasi kikubwa cha mafuta barani Ulaya  ikiwa hali mbaya ya nchi hiyo.Juhudi za kidiplomasia zinaongezeka kufuatia khofu ya kutokea dharura ya nishati.Umoja wa Ulaya unataka kujisghulisha zaidi na mafuta kutoka Nigeria ili kuepuka utegemezi wa nishati ya Urusi.kwa hivyo mhariri wa Handelsblatt anakumbusha kuhusu ziara iliyofanyika hivi karibuni ya mabalozi wa Itali,Ureno,Uhispania Ufaransa na Umoja wa Ulaya walioitembelea kampuni ya mafuta na gesi inayomilikiwa na serikali ya NNPC.Lakini mhariri anasema suali kubwa linaloulizwa ni je ni kiasi gani cha gesi asilia itakayotoka Nigeria katika miaka inayokuja kwa ajili ya Ulaya?Anaendelea kwa kusema hata Brussels hivi sasa inauangalia mpango wa bomba la kupitisha mafuta kutoka Nigeria mpaka Algeria kuwa kitu muhimu cha matumaini.Na kwahakika mipango ya mradi huo ilikuweko tangu miaka ya 1970 hata hivyo mara zote vilizuka vizingiti baadhi ya wakati kulikuweko mivutano kati ya Algeria na Niger na wakati mwingine magenge ya wahuni na magaidi yalifanya vurugu na kuharibu miradi yote ya ujenzi.

die tageszeitung,

Tukamilishe kwa kulitazama gazeti la  Nueu Zürcher ambalo lineandika juu ya mwanaridhiano muingereza mwenye asili ya kisomali aliyejitokeza kumwaga ukweli juu ya asili yake na kisa chake cha kuingia nchini Uingereza. Mo Farah mwanariadha wa mbio ndefu aliiletea shangwe kubwa Uingereza mnamo mwaka 2012 kwa kuiletea medani ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki. Mo Farah mara hii amegonga vichwa vya habari kwa kutangaza kwamba, Mo Farah sio jina lake halisi bali alibadilishwa jina na kusafirishwa kutoka Somalia hadi London alikokuwa muhanga wa kutumikishwa na kufanywa mtumwa.Aliingizwa Uingereza kwa njia za udanganyifu.Mo Farah alisimulia kwamba jina lake hasa ni Hussein Abdi Kahin na alizaliwa Somaliland jimbo lililoko kaskazini mwa Somalia.Kisa hiki pia kimetupiwa jicho na mhariri wa gazeti la di tageszeitung.Na kufikia hapo ndo tunakamilisha udodozi wa magezi ya hapa Ujerumani kuhusu Afrika.