Afrika katika magazeti ya Ujerumani. | Magazetini | DW | 14.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Afrika katika magazeti ya Ujerumani.

Wiki hii magazeti ya Ujerumani yameandika juu ya juhudi za kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zitakazoongozwa na Martin Kobler kutoka Ujerumani Pia yameandika juu ya watoto wa Afrika Magharibi.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,Martin Kobler

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,Martin Kobler

Gazeti la "die tageszeitung" linazingatia juhudi za kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa.Gazeti hilo linatufahamisha kwamba mpango mkubwa kabisa duniani wa Umoja wa Mataifa utaanza kutekelewza mwezi ujao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Gazeti la "die tageszeitung" limearifu kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua mwanadiplomasia wa Ujerumani Martin Kobler kuuongoza mradi huo. Gazeti la "die tageszeitung"limefahamisha kwamba bwana Kobler ameteuliwa kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo .Mjerumani huyo anachukua nafasi ya Mmarekani, Roger Meece aliemaliza muda wake.

Mgogoro wa Mali ,raia wahofia kushambuliwa :

Gazeti la "die tageszeitung"pia limeandika juu ya mgogoro wa Mali.Gazeti hilo limearifu juu ya hofu iliyotanda miongoni mwa watu wanaoitwa" weupe" katika mji wa Timbuktu.

Gazeti hilo linafahamisha zaidi kwa kuandika kwamba Watuareg na Waarabu katika miji iliyokombolewa na majeshi ya Mali kwa kushirikiana na majeshi ya Ufaransa wana hofu kwamba majeshi ya serikali ya Mali yatalipiza kisasi.Gazeti la "die tageszeitung" limezikariri taarifa zinazosema kuwa wakimbizi wengi bado hawajarejea katika mji wa Timbuktu.Gazeti hilo pia limeripoti kwamba taarifa juu ya Watuareg na Waarabu kushambuliwa katika mji wa Timbuktu zinaongezeka.

Gazeti la "die tageszeiutung" limesema kwamba sasa ni vigumu kuwaona Watuareg katika mitaa ya mji waTimbuktu.Jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu hao, gazeti limetoa mfano wa mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 alieumia mguu .Licha ya maumivu makali mzee huyo anaogopa kutoka nje ya nyumba yake ili kutafuta matibabu.

Hata hivyo gazeti la "die tageszeitung" pia limeripoti kwamba wapiganaji wa chama cha Watuareg cha ukombozi wa Azawad,MNLA kimelipiza kisasi kwa kuwashambulia watu wenye rangi nyeusi.

Watoto watumikishwa mashambani:

Ripota wa gazeti la "Neues Deutschland" anaarifu juu ya kutumikishwa kwa watoto kwenye mashamba makubwa ya kakao katika nchi za Afrika magharibi.

Ripota huyo Knut Henkel anaarif kwamba mtindo wa kuwatumia watoto katika kazi za mashambani unazidi kuenea, na hasa katika nchi za Afrika magharibi.Ripota huyo anaeleza katika taarifa yake kwamba wapo mafalahi, yaani wakulima wadogo waodogo, Milioni 5.5 duniani wanaotegemea kilimo cha kakao ili kujiendeshea maisha. Na unapofika wakati wa kuvuna,kazi kubwa inafanywa na watoto.

Ripota huyo anaeleza kuwa hadi kufikia mwaka wa 1980 tani moja ya kakao iliingiza dola alfu tano.Lakini hadi kati kati ya mwaka jana bei ya kakao ilianguka na kufikia dola 2300 kwa tani moja. Kwa hivyo kutokana na bei ya zao hilo kuanguka na kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka wazazi wanawatumia watoto wao kwa kazi nyingi za mashambani.

Mwandishi wa gazeti la "Neues Deutschland"amefahamisha katika taarifa yake kwamba watoto wapatao laki sita wanatumikishwa katika mashamba ya kakao nchini Ghana na Ivory Coast.

"Buruda" wa Ujerumani ahubiri Kenya:

Gazeti la " Süddeutsche" linatupasha habari juu ya mhubiri anaetaka kutumia damu ya Yesu Ksrito,ili kulisafisha bara la Afrika.Gazeti hilo linaeleza kwamba Mhubiri huyo anaitwa Reinhard Bonnke na anafanya kazi ya kuzitibu roho za watu mjini Nairobi. Gazeti hilo limearifu kwamba Mhubiri huyo wa kanisa la Kiprotestanti anawaahidi watu tiba za kimiujiza.

Gazeti la "Süddeutsche" limeripoti kwamba kasisi huyo menye umri wa miaka 73 ametangaza kuwa ufagio wa uokovu utapita nchini Kenya wiki hii na hata wale wenye maradhi ya saratani watapona.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Abdul-Rahman