1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa mkuu wa DFL atangaza kuondoka madarakani 2022

26 Oktoba 2020

Afisa mkuu mtendaji wa Ligi ya soka Ujerumani DFL Christian Seifert ataondoka katika nafasi yake pindi mkataba wake utakapomalizika mwaka 2020, alisema katika taarifa Jumatatu.

https://p.dw.com/p/3kSVB
Fußball Deutschland DLF-Chef Christian Seifert  Video-PK
Picha: picture-alliance/dpa/F. Rumpenhorst

"Hizi ni nyakati zenye changamoto ambazo zinahitaji uwazi na uwezo wa kutegemewa, " alisema Seifert.  Hilo linaihusu pia DFL kwa ujumla na pia kwa malengo yangu ya kitaalamu."

Katika kutangaza uamuzi wake jumatatu, miezi 20 kabla ya kuondoka kwake mnamo juni 30, 2022, Seifert amesema anatarajia kuipa muda wa kutosha bodi ya Ligi ya Soka Ujerumani kujiandaa kwa siku zijazo.

Soma pia: Bosi wa DFL awamwagia sifa mashabiki wa soka Ujerumani

Seifert mwenye umri wa miaka 51, ameiongoza Bundesliga tangu 2005. Chini ya uongozi wake thamani ya mikataba inayuhusiana na matangazio ya televisheni kwa ligi kuu mbili za timu za wataalamu zilifikia kilele cha euro bilioni 4.6 (dola bilioni 5.4)  ongezeko la euro milioni 400 kwa msimu.

Deutschland DFL-Neujahrsempfang in Frankfurt | Christian Seifert
Mkuu wa DFL Christian Seifert.Picha: picture alliance/dpa/A. Dedert

Hata hivyo thamani ya mikataba hiyo imepunguzwa kuanzia msimu wa ligi 2021/22 kwa mika minne ijayo, kutokana na kuzuka kwa janga la virusi vya Corona.

Seifert pamoja na wasimamizi wa ligi ya Ujerumani wamesifiwa kwa taratibu mwafaka za kurudi tena viwanjani baada ya kusitishwa kwa mechi msimu uliopita mwezi machi.

Soma pia: Mashabiki wa soka Ujerumani waonywa

Bundesliga ndio mchuano wa kwanza mkuu kimataifa kurudi viwanjani Mei mwaka huu na mataifa mengine yakifuatilia kwa ukaribu mikakati ya usafi iliyowekwa na Soka la Ujerumani na vilabu mbalimbali.

Hivi karibuni Seifert na DFL pia waliunda jopo kazi kujadili mustakabali wa mpira wa miguu Ujerumani siku zijazo.

"Katika wadfa wangu juu ya bodi ya Ligi ya Soka Ujerumani  DFL, ningeweza kuunda maendeleo ya moja ya ligi kubwa zaidi ya michezo ulimwenguni, taasisi muhimu ya kijamii, na kuanzishwa kwa moja ya kampuni za ubunifu zaidi nchini Ujerumani, "alisema Seifert.

Mnamo Oktoba 17 Seifert alithibitisha kujiuzulu kutoka kamati inayoongoza ya shirikisho la kandanda la Ujerumani (DFB).