Adidas yasitisha udhamini wake na IAAF | Michezo | DW | 26.01.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Adidas yasitisha udhamini wake na IAAF

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Ujerumani Adidas itafikisha mwisho udhamini wake katika shirikisho la vyama vya michezo ya riadha IAAF kiasi miaka minne kabla ya kukamilika kwa mkataba wake

Shirika hilo limeamua dhidi ya kuendelea na mkataba wa udhamini kutokana na kashfa tele katika michezo ya riadha katika matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu misuli yaani doping ambazo zimeibuka Desemba mwaka jana na zimeendelea kulikabili shirikisho hilo.

Shirika hilo linaangalia shutuma hizo za rushwa na doping kuwa ni ukiukaji wa makubaliano ya makataba na IAAF.

Mwaka jana tume huru ya shirika linalopambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu misuli duniani WADA , ilifichua matumizi makubwa ya dawa hizo yaliyokuwa yakidhaminiwa na serikali nchini Urusi. Wiki iliyopita tume hiyo ilitoa sehemu ya pili ya ripoti kuhusiana na uchunguzi wake ambayo inaishutumu IAAF kwa kile ilichosema kuwa ni " kukumbatia rushwa" katika ngazi za juu za shirikisho hilo chini ya rais wake wa zamani Lamine Diack. Diac na mwanae , Papa Massata , wote wako chini ya uchunguzi wa polisi ya Ufaransa kuhusiana na madai ya rushwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / dpae / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com