1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Gedi asema afisa wa WFP ataendelea kuchunguzwa

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EG

Waziri mkuu wa Somalia Ali Mohammed Gedi amesema afisa wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula WFP aliyekamatwa wiki hii na maafisa wa serikali anaendelea kuchunguzwa ingawa hakusema kwanini anachunguzwa.

Akizungumza katika mji mkuu wa Ethiopia waziri mkuu Gedi amewaambia waandishi wa habari kwamba Idriss Osman ikiwa hana hatia ataachiwa mara moja bila ya masharti baada ya kukamilika uchunguzi.

Afisa huyo wa WFP alikamatwa na kutiwa ndani bila ya shirika hilo la Umoja wa mataifa kuarifiwa sababu za kukamatwa kwake.Gedi yuko Ethiopia ambako anakutana na viongizi wa nchi hiyo iliyopeleka wanajeshi na ndege za kivita kuisaidia serikali ya mpito kuwatimua wanamgambo wa mahakama za kiislamu nchini Somalia.