1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Serikali yawasamehe wapinzani waliofungwa maisha.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgj

Serikali ya Ethiopia imesema kuwa imewasamehe na kuwaacha huru mara moja kundi la viongizi wa vyama vya upinzani na wanaharakati.

Waziri mkuu Meles Zenawi amesema kuwa watu hao 38 , ambao walihukumiwa kifungo cha maisha mapema wiki hii, watapata haki zao kamili.

Kurejeshwa kwa haki zao kuna maana kuwa wapinzani hao wa serikali, miongoni mwao wanasiasa, wanaweza kugombea katika chaguzi tena. Mpatanishi katika mzozo huo Profesa Ephrem Isaac amesema kuwa,

hatua za maridhiano zilikwenda vizuri kwasababu serikali pamoja na wafungwa wote waliheshimu utamaduni wetu na wanajua kuwa utamaduni huu wa wazee ni desturi ya muda mrefu nchini Ethiopia. Na watu wa Ethiopia wanaiheshimu na kwamba wale wanaoomba msamaha ni mashujaa na wale wanaotoa msamaha ni watakatifu.

Marekani , mshirika mkubwa wa Ethiopia , imeitaka serikali ya Meles kutoa msamaha huo.

Waziri huyo mkuu amekana kuwa kumekuwa na ushawishi kutoka Marekani katika uamuzi huo. Mahakama kuu ya Ethiopia ilitoa hukumu hiyo ya kifungo cha maisha kwa wajumbe hao wa upinzani kwa kuhusika kwao katika maandamano ya mwaka 2005 ambapo watu kadha wameuwawa.