ADDIS ABABA: Mateka wako salama | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA: Mateka wako salama

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ethiopia, Seyoum Mesfin, amesema wazungu watano na waethiopia wanane waliotekwa nyara na watu waliokuwa na bunduki katika eneo la Afar kaskazini mwa nchi hiyo, wako salama.

Hata hivyo kiongozi huyo hangeweza kuthibitisha ripoti iliyotolewa na kiongozi wa eneo hilo iliyosema watu hao walitekwa nyara na waasi waliojitenga waliowavukisha mpaka na kuingia nchi jirani ya Eritrea.

Kwa upande wake Eritrea inakusha madai hayo kwamba mateka hao waliingizwa katika ardhi yake. Serikali ya Uingereza imesema inachunguza kwa uangalifu mkubwa ripoti hizo kwamba mateka wote wako salama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com