1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Adama Barrow aahidi kuweka ukomo wa muhula wa urais Gambia

8 Desemba 2021

Rais aliyechaguliwa upya nchini Gambia Adama Barrow ameahidi kuweka ukomo wa muhula wa urais kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa pili wa miaka mitano.

https://p.dw.com/p/43z28
Gambia Präsident Adama Barrow kündigt Wahrheitskommission an
Picha: picture-alliance/AP Photo

Barrow, ambaye ushindi wake wa mwaka wa 2016 ulihitimisha zaidi ya miaka 20 ya uongozi wa kidikteta, pia ameiahidi jamii ya kimataifa kuwa atafanya kazi kuhakikisha rais anachaguliwa kwa wingi mkubwa wa kura, badala ya kupitia mfumo wa sasa ambao mgombea anayeshinda kura nyingi katika kila jimbo la uchaguzi anachaguliwa kuwa rais.

Barrow hata hivyo hakuahidi kuwawajibisha wote waliohusika na uhalifu uliofanywa na serikali na mawakala wake chini ya uongozi wa kidikteta wa Yahya Jammeh.

Barrow, ambaye kuchukua kiti cha urais miaka mitano iliyopita kulimaliza zaidi ya miaka 20 ya udikteta, alipata zaidi ya asilimia 53 ya kura, kulingana na matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi. Mpinzani wake mkuu Ousainou Darboe alishika nafasi ya pili na asilimia 27.7.