1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACT-Wazalendo na joto la utawala wa Magufuli

Mohammed Khelef
7 Novemba 2017

Kwenye Kinagaubaga wiki hii, kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, anazungumza na Mohammed Khelef juu ya hali ya kisiasa nchini Tanzania na nafasi ya chama chake kudumu kwenye ulingo wa siasa za vyama vingi katika nyakati kama hizi.

https://p.dw.com/p/2nAaQ

Chama kidogo cha upinzani nchini Tanzania, ACT-Wazalendo, kinaanza kujikuta kwenye msuguano kati yake na vyombo vya dola kwa mara ya mwanzo kabisa kwenye historia, katika wakati ambapo Rais John Magufuli anatimiza miaka miwili ya utawala wake inayoelezwa kuwa migumu sana kwa upinzani na wakosoaji katika taifa hilo kubwa kieneo Afrika Mashariki.